Traducción de los significados del Sagrado Corán - Traducción al idioma swahili- Abdullah Mohamad y Naser Jamis

external-link copy
123 : 7

قَالَ فِرۡعَوۡنُ ءَامَنتُم بِهِۦ قَبۡلَ أَنۡ ءَاذَنَ لَكُمۡۖ إِنَّ هَٰذَا لَمَكۡرٞ مَّكَرۡتُمُوهُ فِي ٱلۡمَدِينَةِ لِتُخۡرِجُواْ مِنۡهَآ أَهۡلَهَاۖ فَسَوۡفَ تَعۡلَمُونَ

Fir'awn akasema kuwaambia wachawi, «Mumemuamini Mwenyezi Mungu kabla sijawapa idhini mumuamini? Hakika kumuamini kwenu Mwenyezi Mungu, kumsadiki kwenu Mūsā na kuukubali kwenu unabii wake ni hila mlizozipanga nyinyi na Mūsā ili muwatoe watu wa mji wenu kutoka humo, na ili muzivamie heri zake na mufaidike nazo peke yenu.Basi mtajua, enyi wachawi, adhabu na mateso yatakayowashukia nyinyi. info
التفاسير: