Traducción de los significados del Sagrado Corán - Traducción al idioma swahili- Abdullah Mohamad y Naser Jamis

external-link copy
31 : 6

قَدۡ خَسِرَ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِلِقَآءِ ٱللَّهِۖ حَتَّىٰٓ إِذَا جَآءَتۡهُمُ ٱلسَّاعَةُ بَغۡتَةٗ قَالُواْ يَٰحَسۡرَتَنَا عَلَىٰ مَا فَرَّطۡنَا فِيهَا وَهُمۡ يَحۡمِلُونَ أَوۡزَارَهُمۡ عَلَىٰ ظُهُورِهِمۡۚ أَلَا سَآءَ مَا يَزِرُونَ

Hakika wamepata hasara wale waliokanusha kufufuliwa baada ya kufa. Mpaka Kiyama kitakaposimama na wakashutushwa kwa mwisho mbaya, watazipigia nafsi zao kelele za majuto juu ya kile walichokipoteza katika maisha yao ya ulimwenguni, hali ya kwamba wanabeba madhambi yao juu ya migongo yao. Ni mibaya iliyoje mizigo hiyo mizito iliyo miovu ambayo wataibeba! info
التفاسير: