Traducción de los significados del Sagrado Corán - Traducción al idioma swahili- Abdullah Mohamad y Naser Jamis

external-link copy
21 : 6

وَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّنِ ٱفۡتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا أَوۡ كَذَّبَ بِـَٔايَٰتِهِۦٓۚ إِنَّهُۥ لَا يُفۡلِحُ ٱلظَّٰلِمُونَ

Hakuna yoyote mwenye udhalimu mbaya zaidi kuliko yule aliyemzulia Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, urongo na akadai kwamba Yeye Ana washirika katika ibada, au akadai kwamba Yeye Ana mtoto au mke, au akazikanusha hoja Zake na dalili ambazo kwazo Aliwapa nguvu Mitume Wake, amani iwashukie. Hakika ya mambo ni kwamba madhalimu waliomzulia Mwenyezi Mungu urongo hawafaulu na hawapati matakwa yao ulimwenguni wala Akhera. info
التفاسير: