Traducción de los significados del Sagrado Corán - Traducción al idioma swahili- Abdullah Mohamad y Naser Jamis

external-link copy
136 : 6

وَجَعَلُواْ لِلَّهِ مِمَّا ذَرَأَ مِنَ ٱلۡحَرۡثِ وَٱلۡأَنۡعَٰمِ نَصِيبٗا فَقَالُواْ هَٰذَا لِلَّهِ بِزَعۡمِهِمۡ وَهَٰذَا لِشُرَكَآئِنَاۖ فَمَا كَانَ لِشُرَكَآئِهِمۡ فَلَا يَصِلُ إِلَى ٱللَّهِۖ وَمَا كَانَ لِلَّهِ فَهُوَ يَصِلُ إِلَىٰ شُرَكَآئِهِمۡۗ سَآءَ مَا يَحۡكُمُونَ

Na wale wenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka na kuwa juu, waliziweka kando sehemu ya vitu Alivyoviumba miongoni mwa mazao, matunda na wanyama howa wakawapatia wageni na maskini; na wakaziweka kando sehemu nyingine za vitu hivi kwa washirika wao, miongoni mwa masanamu na mizimu. Basi zile zilizotengewa washirika wao zafikishwa kwao peke yao, na hazifiki kwa Mwenyezi Mungu; na zile zilizotengewa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, zinafika kwa washirika wao. Ni mbaya ulioje uaumuzi wa hao watu na kigawanyo chao. info
التفاسير: