Traducción de los significados del Sagrado Corán - Traducción al idioma swahili- Abdullah Mohamad y Naser Jamis

Número de página:close

external-link copy
95 : 6

۞ إِنَّ ٱللَّهَ فَالِقُ ٱلۡحَبِّ وَٱلنَّوَىٰۖ يُخۡرِجُ ٱلۡحَيَّ مِنَ ٱلۡمَيِّتِ وَمُخۡرِجُ ٱلۡمَيِّتِ مِنَ ٱلۡحَيِّۚ ذَٰلِكُمُ ٱللَّهُۖ فَأَنَّىٰ تُؤۡفَكُونَ

Hakika Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Anapasua mbegu ukatoka mmea, na Anapasua koko ukatoka mti. Anatoa chenye uhai kutokana na kilichokufa, kama vile binadamu na mnyama kutokana na tone la manii ya binadamu na mnyama. Na Anatoa kilichokufa kutokana na chenye uhai, kama tone la manii linalotokana na binadamu na mnyama. Huyo Ndiye Mwenyezi Mungu. Yaani Mwenye kufanya hili ni Mwenyezi Mungu, Peke Yake, Asiye na mshirika, Anayestahiki kuabudiwa. Basi vipi nyinyi mtaepushwa na haki mpelekwe kwenye batili mkamuabudu pamoja na Yeye mwingine asiyekuwa Yeye? info
التفاسير:

external-link copy
96 : 6

فَالِقُ ٱلۡإِصۡبَاحِ وَجَعَلَ ٱلَّيۡلَ سَكَنٗا وَٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَ حُسۡبَانٗاۚ ذَٰلِكَ تَقۡدِيرُ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡعَلِيمِ

Na Mwenyezi Mungu, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, Ndiye Ambaye Alipasua mwangaza wa asubuhi kutoka kwenye giza la usiku, na Akaufanya usiku ni wakati wa utulivu, anatulia humo anayechoka mchana na kupata fungu lake la mapumziko, na Akalifanya jua na mwezi zinatembea katika njia zake kwa hesabu ya sawsawa iliyokadiriwa, haibadiliki wala haigongani. Hayo ndiyo makadirio ya Al- ’Azīz, Mwenye kushinda, ambaye ufalme Wake umeshinda, Al- ’Alīm, Aliye Mjuzi wa maslahi ya viumbe Wake na kuendesha mambo yao. Al- ’Azīz na Al- ’Alīm ni miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu mazuri yanayoonesha ukamilifu wa ushindi na ujuzi. info
التفاسير:

external-link copy
97 : 6

وَهُوَ ٱلَّذِي جَعَلَ لَكُمُ ٱلنُّجُومَ لِتَهۡتَدُواْ بِهَا فِي ظُلُمَٰتِ ٱلۡبَرِّ وَٱلۡبَحۡرِۗ قَدۡ فَصَّلۡنَا ٱلۡأٓيَٰتِ لِقَوۡمٖ يَعۡلَمُونَ

Na Mwenyezi Mungu, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, Ndiye Aliyewawekea, enyi watu, nyota ni alama ya nyinyi kujua njia kipindi cha usiku mnapopotea kwa sababu ya giza lingi, barani na baharini. Tumezifafanua hoja zilizo wazi, ili wazizingatie miongoni mwenu wenye elimu ya kumjua Mwenyezi Mungu na sheria Yake. info
التفاسير:

external-link copy
98 : 6

وَهُوَ ٱلَّذِيٓ أَنشَأَكُم مِّن نَّفۡسٖ وَٰحِدَةٖ فَمُسۡتَقَرّٞ وَمُسۡتَوۡدَعٞۗ قَدۡ فَصَّلۡنَا ٱلۡأٓيَٰتِ لِقَوۡمٖ يَفۡقَهُونَ

Na Mwenyezi Mungu, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, Ndiye Aliyeanza kuwaumba, enyi watu, kutokana na Ādam, amani imshukiye, Alipomuumba kwa udongo, kisha mkawa nyinyi ni kizazi chenye kuendelea kutokana na yeye, Akawafanyia kituo cha nyinyi kutulia, nacho ni zao za wanawake; na Akawafanyia hazina ya nyinyi kuhifadhiwa , nayo ni migongo ya wanaume. Tumeshawabainishia hoja na kuwapambanulia dalili na kuzithibitisha kwa watu wenye kufahamu vituo vya hoja na sehemu za mazingatio. info
التفاسير:

external-link copy
99 : 6

وَهُوَ ٱلَّذِيٓ أَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ فَأَخۡرَجۡنَا بِهِۦ نَبَاتَ كُلِّ شَيۡءٖ فَأَخۡرَجۡنَا مِنۡهُ خَضِرٗا نُّخۡرِجُ مِنۡهُ حَبّٗا مُّتَرَاكِبٗا وَمِنَ ٱلنَّخۡلِ مِن طَلۡعِهَا قِنۡوَانٞ دَانِيَةٞ وَجَنَّٰتٖ مِّنۡ أَعۡنَابٖ وَٱلزَّيۡتُونَ وَٱلرُّمَّانَ مُشۡتَبِهٗا وَغَيۡرَ مُتَشَٰبِهٍۗ ٱنظُرُوٓاْ إِلَىٰ ثَمَرِهِۦٓ إِذَآ أَثۡمَرَ وَيَنۡعِهِۦٓۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكُمۡ لَأٓيَٰتٖ لِّقَوۡمٖ يُؤۡمِنُونَ

Na Mwenyezi Mungu, kutakata na sifa za pungufu ni Kwake, Nadiye Aliyetaramsha mvua kutoka kwenye mawingu, Akatoa kwayo mimea ya kila kitu, Akatoa, kutokana na mimea, nafaka na miti mibichi, kisha akatoa kwenye mimea ya nafaka mbegu zilizoshikana, kama masuke ya mahindi, ngano na mpunga. Na Akatoa kutoka kwenye kizao cha mtende, nacho ni kile ambacho karara la tende linachomoza hapo, mitungo ambayo kuitunda ni karibu. Na Akatoa, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, mashamba ya mizabibu. Na Akatoa mizaituni na mikomamanga ambayo majani yake yanafanana na matunda yake yanatafautiana kimaumbile, uatamu na kitabia. Angalieni, enyi watu, matunda ya mimea hii inapotoa mazao na kuiva kwake na kustawi kwake yanapostawi. Hakika katika hayo, enyi watu, kuna dalili ya ukamilifu wa uwezo wa muumba vitu hivi, hekima Yake na rehema Yake kwa watu wenye kumuamini Yeye, Aliyetukuka, na kuzifuata sheria Yake kivitendo. info
التفاسير:

external-link copy
100 : 6

وَجَعَلُواْ لِلَّهِ شُرَكَآءَ ٱلۡجِنَّ وَخَلَقَهُمۡۖ وَخَرَقُواْ لَهُۥ بَنِينَ وَبَنَٰتِۭ بِغَيۡرِ عِلۡمٖۚ سُبۡحَٰنَهُۥ وَتَعَٰلَىٰ عَمَّا يَصِفُونَ

Na hawa washirikina wamefanya majini ni washirika wa Mwenyezi Mungu katika ibada, kwa kuitakidi kwao kuwa wao wanalete manufaa au madhara, na hali Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Amewaumba wao na wanavyoviabudu kutoka kwenye ‘adam ( hali ya kutokuwako). Basi ni Yeye Aliyepwkeka kwa kuumba, Peke Yake, na inapasa Apwekeke kwa kuabudiwa Peke Yake, Asiye na mshirika. Na, kwa kweli, hawa washirikina walisema urongo kumzulia Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, walipomnasibishia Yeye watoto wa kiume na wakike, kwa kutojua kwao sifa Zake za ukamilifu zinazompasa. Ameepuka na kuwa juu ya yale, ambayo walimnasibisha nayo washirikina, ya urongo na uzushi. info
التفاسير:

external-link copy
101 : 6

بَدِيعُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ أَنَّىٰ يَكُونُ لَهُۥ وَلَدٞ وَلَمۡ تَكُن لَّهُۥ صَٰحِبَةٞۖ وَخَلَقَ كُلَّ شَيۡءٖۖ وَهُوَ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمٞ

Na Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Ndiye Aliyezipatisha mbingu na ardhi na vilivyomo humo, kwa namna isiyokuwa na mfano uliotangulia. Vipi Awe na mtoto, na hakuwa na mke? Ametukuka Mwenyezi Mungu kutukuka kukubwa na yale wanayoyasema washirikina, Na Yeye Ndiye Aliyeumba kila kitu kutokana na hali ya kutokuwako na hakuna chochote chenye kufichika Kwake katika mambo ya viumbe. info
التفاسير: