Traducción de los significados del Sagrado Corán - Traducción al idioma swahili- Abdullah Mohamad y Naser Jamis

Qamar

external-link copy
1 : 54

ٱقۡتَرَبَتِ ٱلسَّاعَةُ وَٱنشَقَّ ٱلۡقَمَرُ

Kimekaribia Kiyama na mwezi umepasuka pande mbili, pale makafiri wa Makkah walipomtaka Nabii, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshikie, awaoneshe alama, na yeye akamuomba Mwenyezi Mungu na akawaonesha hiyo alama. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 54

وَإِن يَرَوۡاْ ءَايَةٗ يُعۡرِضُواْ وَيَقُولُواْ سِحۡرٞ مُّسۡتَمِرّٞ

Na washirikina wakiiona dalili na ushahidi juu ya ukweli wa Mtume Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, wanakataa kuziamini na kuzisadiki hali ya kukanusha na kupinga, na wanasema baada ya dalili kujitokeza, «Huu ni uchawi wenye ubatilifu na wenye kuondoka na kupotea usiokuwa na sifa ya kudumu. info
التفاسير:

external-link copy
3 : 54

وَكَذَّبُواْ وَٱتَّبَعُوٓاْ أَهۡوَآءَهُمۡۚ وَكُلُّ أَمۡرٖ مُّسۡتَقِرّٞ

Na walimkanusha Nabii, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, wakafuata upotevu wao na kile cha ukanushaji ambacho matamanio yao yaliwavuta kwacho. Na kila jambo, la kheri au la shari, litawashukia wanaostahili Siku ya Kiyama yatakapodhihiri malipo na mateso. info
التفاسير:

external-link copy
4 : 54

وَلَقَدۡ جَآءَهُم مِّنَ ٱلۡأَنۢبَآءِ مَا فِيهِ مُزۡدَجَرٌ

Na hakika ziliwajia makafiri wa Kikureshi habari za ummah waliokanusha mitume wao na adhabu iliyowashukia zinazotosha kuwakemea na kuwafanya warudi nyuma waache ukafiri wao na upotevu wao. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 54

حِكۡمَةُۢ بَٰلِغَةٞۖ فَمَا تُغۡنِ ٱلنُّذُرُ

Hii Qur’ani iliowajia ni hekima kubwa iliyofikia upeo. Basi yatawafalia nini maonyo wale watu waliyoipa mgongo na kuikanusha? info
التفاسير:

external-link copy
6 : 54

فَتَوَلَّ عَنۡهُمۡۘ يَوۡمَ يَدۡعُ ٱلدَّاعِ إِلَىٰ شَيۡءٖ نُّكُرٍ

Kwa hivyo, wapuuze, ewe Mtume, na uingojee Siku kubwa, Siku Malaika Atakapoita, kwa kuvuvia kwenye baragumu, kwenye jambo linalotisha linalochukiza, nalo ni Kisimamo cha Hesabu. info
التفاسير:

external-link copy
7 : 54

خُشَّعًا أَبۡصَٰرُهُمۡ يَخۡرُجُونَ مِنَ ٱلۡأَجۡدَاثِ كَأَنَّهُمۡ جَرَادٞ مُّنتَشِرٞ

Hali yakuwa macho yao yamedhalilika, wanatoka makaburini kama kwamba wao kwa kuenea kwao na upesi wa kuenda kwenye kuhesabiwa, ni nzige walioenea pambizoni mwa anga, info
التفاسير:

external-link copy
8 : 54

مُّهۡطِعِينَ إِلَى ٱلدَّاعِۖ يَقُولُ ٱلۡكَٰفِرُونَ هَٰذَا يَوۡمٌ عَسِرٞ

hali ya kukimbilia kile walichoitiwa. Hapo waseme makafiri, «Hii ni siku nzito yenye vituko vikubwa.» info
التفاسير:

external-link copy
9 : 54

۞ كَذَّبَتۡ قَبۡلَهُمۡ قَوۡمُ نُوحٖ فَكَذَّبُواْ عَبۡدَنَا وَقَالُواْ مَجۡنُونٞ وَٱزۡدُجِرَ

Walikanusha kabla ya watu wako, ewe Mtume, watu wa Nūḥ wakamkanusha mja wetu Nūḥ na wakasema, «Yeye ni Mwendawazimu.» Wakamkaripia huku wakimtisha kwa aina nyingi za mateso iwapo hatakomeka na ulinganizi wake. info
التفاسير:

external-link copy
10 : 54

فَدَعَا رَبَّهُۥٓ أَنِّي مَغۡلُوبٞ فَٱنتَصِرۡ

Nūḥ akamuomba Mola wake kwamba «mimi ni dhaifu wa kupambana na hawa, basi nisaidie mimi kwa kuwapa mateso yanayotoka kwako kwa kukukanusha wewe.» info
التفاسير:

external-link copy
11 : 54

فَفَتَحۡنَآ أَبۡوَٰبَ ٱلسَّمَآءِ بِمَآءٖ مُّنۡهَمِرٖ

Basi tukayakubali maombi yake, na tukafungua milango ya mbingu kwa maji mengi yenye kuteremka kwa nguvu, info
التفاسير:

external-link copy
12 : 54

وَفَجَّرۡنَا ٱلۡأَرۡضَ عُيُونٗا فَٱلۡتَقَى ٱلۡمَآءُ عَلَىٰٓ أَمۡرٖ قَدۡ قُدِرَ

na tukapasua ardhi tukatoa chemchemi za maji yanayotoka kwa kasi, yakakutana maji ya mbinguni na maji ya ardhini kuwaangamiza wao kwa vile Alivyowakadiria mwenyezi Mungu, yakiwa ni malipo ya ushirikina wao. info
التفاسير:

external-link copy
13 : 54

وَحَمَلۡنَٰهُ عَلَىٰ ذَاتِ أَلۡوَٰحٖ وَدُسُرٖ

Tukambeba Nūḥ na waliokuwa pamoja naye juu ya jahazi ya mbao zilizopigwa misumari, info
التفاسير:

external-link copy
14 : 54

تَجۡرِي بِأَعۡيُنِنَا جَزَآءٗ لِّمَن كَانَ كُفِرَ

ikawa inatembea kwa uangalizi wetu na utunzi, na tukawazamisha waliokanusha, ikiwa ni malipo yao kwa ukafiri wao na kwa kumnusuru Nūḥ, amani imshukie. Hapa pana dalili ya kuthibitisha sifa ya macho mawili kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kutukuka, kama inavyonasibiana na Yeye. info
التفاسير:

external-link copy
15 : 54

وَلَقَد تَّرَكۡنَٰهَآ ءَايَةٗ فَهَلۡ مِن مُّدَّكِرٖ

Na kwa hakika tulikibakisha kisa cha Nūḥ pamoja na watu wake kiwe ni mazingatio na dalili ya uweza wetu kwa walio baada ya Nūḥ, ili wazingatie na wawaidhike kwa lililowapata ummah huu uliokanusha Mtume wao, info
التفاسير:

external-link copy
16 : 54

فَكَيۡفَ كَانَ عَذَابِي وَنُذُرِ

basi je kuna wakuwaidhika awaidhike? Na ilikuwa vipi adhabu yangu na maonyo yangu kwa aliyenikufuru mimi, akawakanusha Mitume wangu na asiwaidhike kwa walichokuja nacho? Hakika hiyo ilikuwa kubwa yenye uchungu. info
التفاسير:

external-link copy
17 : 54

وَلَقَدۡ يَسَّرۡنَا ٱلۡقُرۡءَانَ لِلذِّكۡرِ فَهَلۡ مِن مُّدَّكِرٖ

Kwa hakika tumeyasahilisha matamko ya Qur’ani ili isomwe na ihifadhiwe, na pia maana yake ili ieleweke na izingatiwe. Je kuna mwenye kuwaidhika nayo? Katika aya hii na mfano wake katika hii Sura kuna kuhimiza kusoma Qur’ani kwa wingi, kujifunza na kuifundisha. info
التفاسير:

external-link copy
18 : 54

كَذَّبَتۡ عَادٞ فَكَيۡفَ كَانَ عَذَابِي وَنُذُرِ

Watu wa kabila la 'Ād walimkanusha Hūd tukawatesa, basi ilikuwa vipi vile nilivyowaadhibu wao kwa ukafiri wao na vile nilivyowaonya wao kwa kumkanusha Mtume wao na kutomuamini? Ilikuwa kubwa yenye uchungu. info
التفاسير:

external-link copy
19 : 54

إِنَّآ أَرۡسَلۡنَا عَلَيۡهِمۡ رِيحٗا صَرۡصَرٗا فِي يَوۡمِ نَحۡسٖ مُّسۡتَمِرّٖ

Hakika sisi tuliwapelekea upepo wenye baridi kali katika siku korofi yenye kuendelea kwao kwa adhabu na maangamivu, info
التفاسير:

external-link copy
20 : 54

تَنزِعُ ٱلنَّاسَ كَأَنَّهُمۡ أَعۡجَازُ نَخۡلٖ مُّنقَعِرٖ

yenye kung’oa watu kutoka mahali walipo kwenye ardhi na kuwatupa kwa vichwa vyao, kuzivunja shingo zao na kuvipambanua vichwa vyao na miili yao na kuwaacha kama mitende iliyong’olewa kutoka mashinani. info
التفاسير:

external-link copy
21 : 54

فَكَيۡفَ كَانَ عَذَابِي وَنُذُرِ

Basi ilikuwa vipi adhabu yangu na onyo langu kwa aliyenikufuru na akawakanusha Mitume wangu na Asiwaamini? Hakika ilikuwa kubwa yenye uchungu! info
التفاسير:

external-link copy
22 : 54

وَلَقَدۡ يَسَّرۡنَا ٱلۡقُرۡءَانَ لِلذِّكۡرِ فَهَلۡ مِن مُّدَّكِرٖ

Na kwa hakika tumeyasahilisha matamko ya Qur’ani, ili isomwe na ihifadhiwe, na tumeyasahilisha maana yake, ili ieleweke na izingatiwe kwa anayetaka kuwaaidhika na kuzingatia. Je kuna yoyote mwenye kuwaidhika nayo? Hapa pana kuhimiza kusoma Qur’ani kwa wingi, kujifunza na kufundisha. info
التفاسير:

external-link copy
23 : 54

كَذَّبَتۡ ثَمُودُ بِٱلنُّذُرِ

Walizikanusha watu wa kabila la Thamūd, nao ni watu wa Ṣāliḥ, alama ambazo walionywa nazo, info
التفاسير:

external-link copy
24 : 54

فَقَالُوٓاْ أَبَشَرٗا مِّنَّا وَٰحِدٗا نَّتَّبِعُهُۥٓ إِنَّآ إِذٗا لَّفِي ضَلَٰلٖ وَسُعُرٍ

wakasema, «Je tumfuate binadamu mmoja miongoni mwetu na hali sisi ni wengi na yeye ni mmoja? Tukifanya hivyo tutakuwa mbali na usawa na tutakuwa ni wenye wazimu. info
التفاسير:

external-link copy
25 : 54

أَءُلۡقِيَ ٱلذِّكۡرُ عَلَيۡهِ مِنۢ بَيۡنِنَا بَلۡ هُوَ كَذَّابٌ أَشِرٞ

«Je Ameteremshiwa wahyi na kuhusishwa yeye pekee kwa utume miongoni mwetu, na hali yeye ni mmoja katika sisi? Bali yeye ana urongo mwingi na kiburi.» info
التفاسير:

external-link copy
26 : 54

سَيَعۡلَمُونَ غَدٗا مَّنِ ٱلۡكَذَّابُ ٱلۡأَشِرُ

Basi wataona wakati wa adhabu kuwateremkia hapa duniani na huko Akhera, ni nani mrongo mwenye kiburi? info
التفاسير:

external-link copy
27 : 54

إِنَّا مُرۡسِلُواْ ٱلنَّاقَةِ فِتۡنَةٗ لَّهُمۡ فَٱرۡتَقِبۡهُمۡ وَٱصۡطَبِرۡ

Sisi tutamtoa ngamia waliomtaka kutoka kwenye jiwe, huo ukiwa ni mtihani kwao. Basi ingojee, ewe Ṣāliḥ, adhabu itakaowashukia, na usubiri katika kuwalingania na juu ya makero wanayokufanyia. info
التفاسير:

external-link copy
28 : 54

وَنَبِّئۡهُمۡ أَنَّ ٱلۡمَآءَ قِسۡمَةُۢ بَيۡنَهُمۡۖ كُلُّ شِرۡبٖ مُّحۡتَضَرٞ

Na uwape habari kwamba maji yamegawanywa baina ya watu wako na ngamia: ngamia ana siku yake na nyinyi mna siku yenu, kila siku ya kunywa atakuja yule ambaye ni siku yake aliyogawanyiwa, na atakatazwa yule ambaye si siku yake aliyogawanyiwa. info
التفاسير:

external-link copy
29 : 54

فَنَادَوۡاْ صَاحِبَهُمۡ فَتَعَاطَىٰ فَعَقَرَ

Wakamuita mwenzao wakimshawishi amchinje, basi akamshika yule ngamia kwa mkono wake na akamchinja, na mimi nikawatesa, info
التفاسير:

external-link copy
30 : 54

فَكَيۡفَ كَانَ عَذَابِي وَنُذُرِ

basi ilikuwa vipi nilivyowaadhibu kwa ukafiri wao na nilivyowaonya waliowaasi Mitume wangu? Hakika hiyo ilikuwa adhabu kubwa yenye uchungu. info
التفاسير:

external-link copy
31 : 54

إِنَّآ أَرۡسَلۡنَا عَلَيۡهِمۡ صَيۡحَةٗ وَٰحِدَةٗ فَكَانُواْ كَهَشِيمِ ٱلۡمُحۡتَظِرِ

Sisi tuliwateremshia Jibrili, akawapigia ukulele mmoja, wakatoeka hadi wa mwisho wao, wakawa ni kama nyasi zilizokauka zilizo nyepesi kuvunjika, zinazofanyiwa boma la ngamia na mifugo. info
التفاسير:

external-link copy
32 : 54

وَلَقَدۡ يَسَّرۡنَا ٱلۡقُرۡءَانَ لِلذِّكۡرِ فَهَلۡ مِن مُّدَّكِرٖ

Na kwa hakika tumeyasahilisha matamko ya Qur’ani, ili isomwe na ihifadhiwe, na tumeyasahilisha maana yake, ili ifahamike na izingatiwe kwa anayetaka kuwaidhika na kuzingatia. Basi je kuna yoyote mwenye kuwaidhika nayo? info
التفاسير:

external-link copy
33 : 54

كَذَّبَتۡ قَوۡمُ لُوطِۭ بِٱلنُّذُرِ

Walizikanusha watu wa Lūṭ aya za Mwenyezi Mungu walioonywa nazo. info
التفاسير:

external-link copy
34 : 54

إِنَّآ أَرۡسَلۡنَا عَلَيۡهِمۡ حَاصِبًا إِلَّآ ءَالَ لُوطٖۖ نَّجَّيۡنَٰهُم بِسَحَرٖ

Sisi tuliwateremshia upepo mkali unaowarushia mawe, isipokuwa watu wa Lūṭ wa nyumbani, kwani wao tuliwaokoa na adhabu kipindi cha mwisho wa usiku, info
التفاسير:

external-link copy
35 : 54

نِّعۡمَةٗ مِّنۡ عِندِنَاۚ كَذَٰلِكَ نَجۡزِي مَن شَكَرَ

ikiwa ni neema itokayo kwetu juu yao. Kama tulivyompa malipo mema Lūṭ na watu wake wa nyumbani, tukawapa neema na tukawaokoa na adhabu yetu ndivyo tunavyowalipa mema waliotuamini na kutushukuru. info
التفاسير:

external-link copy
36 : 54

وَلَقَدۡ أَنذَرَهُم بَطۡشَتَنَا فَتَمَارَوۡاْ بِٱلنُّذُرِ

Kwa hakika Lūṭ aliwaonya watu wake mateso ya Mwenyezi Mungu na adhabu Yake, wasimsikilize, bali walilifanyia shaka hilo na wakamkanusha. info
التفاسير:

external-link copy
37 : 54

وَلَقَدۡ رَٰوَدُوهُ عَن ضَيۡفِهِۦ فَطَمَسۡنَآ أَعۡيُنَهُمۡ فَذُوقُواْ عَذَابِي وَنُذُرِ

Na kwa hakika walitaka kwake kufanya uchafu na wageni wake ambao ni Malaika, tukayafuta macho yao wasione chochote na wakaambiwa, «Onjeni adhabu yangu na onyo langu alilowaonya nalo Lūṭ, amani imshukie.» info
التفاسير:

external-link copy
38 : 54

وَلَقَدۡ صَبَّحَهُم بُكۡرَةً عَذَابٞ مُّسۡتَقِرّٞ

Na iliwajia kipindi cha asubuhi adhabu ya kuendelea, imejikita kwao mpaka iwafikishe kwenye adhabu ya Akhera. Adhabu yenyewe ni kuvurumizwa mawe na kuipindua miji yao kwa namna ambayo kulikokuwa juu kukawa chini, info
التفاسير:

external-link copy
39 : 54

فَذُوقُواْ عَذَابِي وَنُذُرِ

na wakaambiwa, «Onjeni adhabu yangu niliyowateremshia nyinyi kwa sababu ya ukafiri wenu na ukanushaji wenu onyo langu alilowaonya nalo Lūṭ, amani imshukie. info
التفاسير:

external-link copy
40 : 54

وَلَقَدۡ يَسَّرۡنَا ٱلۡقُرۡءَانَ لِلذِّكۡرِ فَهَلۡ مِن مُّدَّكِرٖ

Na kwa hakika tumeyasahilisha matamko ya Qur’ani, ili isomwe na ihifadhiwe, na tumeyasahilisha maana yake, ili ifahamike na izingatiwe kwa anayetaka kuwaidhika na kuzingatia. Basi je kuna mwenye kuwaidhika nayo? info
التفاسير:

external-link copy
41 : 54

وَلَقَدۡ جَآءَ ءَالَ فِرۡعَوۡنَ ٱلنُّذُرُ

Kwa hakika lilimjia Fir'awn na watu wake onyo letu la kuwatesa kwa ukafiri wao. info
التفاسير:

external-link copy
42 : 54

كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا كُلِّهَا فَأَخَذۡنَٰهُمۡ أَخۡذَ عَزِيزٖ مُّقۡتَدِرٍ

Walizikanusha dalili zetu zote zenye kutolea ushahidi upweke wetu na unabii wa Manabii wetu, tukawatesa kwa adhabu mateso ya Mshindi Asiyeshindwa, Mweza wa Analolitaka. info
التفاسير:

external-link copy
43 : 54

أَكُفَّارُكُمۡ خَيۡرٞ مِّنۡ أُوْلَٰٓئِكُمۡ أَمۡ لَكُم بَرَآءَةٞ فِي ٱلزُّبُرِ

Je makafiri wenu, enyi mkusanyiko wa Makureshi, ni bora kuliko wale waliotangulia kutajwa miongoni mwa wale walioangamia kwa sababu ya kukanusha kwao? Au nyinyi mmeepushwa na mateso ya Mwenyezi Mungu kwa yaliyomo kwenye Vitabu vilivyoteremshwa kwa Mitume kwa kuwa mtasalimika na mateso? info
التفاسير:

external-link copy
44 : 54

أَمۡ يَقُولُونَ نَحۡنُ جَمِيعٞ مُّنتَصِرٞ

Au kwani wanasema makafiri wa Makkah, «Sisi ndio wenye ushupavu na busara, na jambo letu ni la pamoja. Sisi ni watu wa ushindi, na hatatushinda anayetutaka kwa ubaya.?» info
التفاسير:

external-link copy
45 : 54

سَيُهۡزَمُ ٱلۡجَمۡعُ وَيُوَلُّونَ ٱلدُّبُرَ

Utashindwa mkusanyiko wa makafiri wa Makkah mbele ya Waislamu na watakimbia. Na hili lilitokea siku ya vita vya Badr. info
التفاسير:

external-link copy
46 : 54

بَلِ ٱلسَّاعَةُ مَوۡعِدُهُمۡ وَٱلسَّاعَةُ أَدۡهَىٰ وَأَمَرُّ

Na wakati wa Kiyama ambao ndio agizo la wao kulipwa wanachostahiki, na Wakati wa Kiyama ni mkubwa na mgumu zaidi kuliko adhabu iliyowafika siku ya Badr. info
التفاسير:

external-link copy
47 : 54

إِنَّ ٱلۡمُجۡرِمِينَ فِي ضَلَٰلٖ وَسُعُرٖ

Hakika wahalifu wa ukafiri wako katika hali ya kuduwaa kutoijua haki na wako kwenye usumbufu na adhabu. info
التفاسير:

external-link copy
48 : 54

يَوۡمَ يُسۡحَبُونَ فِي ٱلنَّارِ عَلَىٰ وُجُوهِهِمۡ ذُوقُواْ مَسَّ سَقَرَ

Siku watakapokokotwa ndani ya Moto kwa nyuso zao na waambiwe, «Onjeni ukali wa adhabu ya moto wa Jahanamu.» info
التفاسير:

external-link copy
49 : 54

إِنَّا كُلَّ شَيۡءٍ خَلَقۡنَٰهُ بِقَدَرٖ

Hakika sisi kila kitu tumekiumba kwa kipimo tulichokikadiri na kukipitisha, na ilitangulia elimu yetu ya kukijua kitu hiko na kukiandika kwenye Ubao Uliohifadhiwa. info
التفاسير:

external-link copy
50 : 54

وَمَآ أَمۡرُنَآ إِلَّا وَٰحِدَةٞ كَلَمۡحِۭ بِٱلۡبَصَرِ

Na haikuwa amri yetu ya kuamuru jambo tukitaka liwe isipokuwa ni kuliambia neno moja nalo ni «kuwa» nalo likawa palepale kama vile kupeleka jicho kuangalia kitu, haichelewi hata kiasi cha jicho kupepesa. info
التفاسير:

external-link copy
51 : 54

وَلَقَدۡ أَهۡلَكۡنَآ أَشۡيَاعَكُمۡ فَهَلۡ مِن مُّدَّكِرٖ

Na kwa hakika tuliwaangamiza wale waliofanana na nyinyi katika ukafiri miongoni mwa ummah waliopita. Basi je, kuna mwenye kuwaidhika kwa mateso na adhabu? info
التفاسير:

external-link copy
52 : 54

وَكُلُّ شَيۡءٖ فَعَلُوهُ فِي ٱلزُّبُرِ

Na kila kitu walichokifanya wale wanaofanana na nyinyi waliopita, cha kheri au cha shari, kimeandikwa kwenye Vitabu ambavyo Malaika watunzi wenye kudhibiti waliviandika. info
التفاسير:

external-link copy
53 : 54

وَكُلُّ صَغِيرٖ وَكَبِيرٖ مُّسۡتَطَرٌ

Na kila dogo au kubwa katika matendo yao limesajiliwa ndani ya madaftari yao, na watalipwa kwayo. info
التفاسير:

external-link copy
54 : 54

إِنَّ ٱلۡمُتَّقِينَ فِي جَنَّٰتٖ وَنَهَرٖ

Hakika wachamungu watakuwa kwenye mabustani ya Pepo makubwa na mito mipana Siku ya Kiyama. info
التفاسير:

external-link copy
55 : 54

فِي مَقۡعَدِ صِدۡقٍ عِندَ مَلِيكٖ مُّقۡتَدِرِۭ

Kwenye kikao cha haki, kisochokuwa na maneno ya upuuzi wala ya kuwatia madhambini, mbele ya Mwenyezi Mungu, Aliye Mfalme Mkubwa, Muumba vitu vyote, Mwenye uweza wa kila kitu, Aliyetukuka na kuwa juu. info
التفاسير: