Traducción de los significados del Sagrado Corán - Traducción al idioma swahili- Abdullah Mohamad y Naser Jamis

Número de página:close

external-link copy
26 : 40

وَقَالَ فِرۡعَوۡنُ ذَرُونِيٓ أَقۡتُلۡ مُوسَىٰ وَلۡيَدۡعُ رَبَّهُۥٓۖ إِنِّيٓ أَخَافُ أَن يُبَدِّلَ دِينَكُمۡ أَوۡ أَن يُظۡهِرَ فِي ٱلۡأَرۡضِ ٱلۡفَسَادَ

Na Fir'awn alisema kuwaambia watukufu wa watu wake, «Niacheni nimuue Mūsā, na amuombe Mola wake, anayedai kuwa Yeye Amemtumiliza kwetu, Amhifadhi na sisi. Mimi ninachelea asije akaigeuza dini yenu mliyonayo au asije akaeneza uharibifu kwenye ardhi ya Misri.» info
التفاسير:

external-link copy
27 : 40

وَقَالَ مُوسَىٰٓ إِنِّي عُذۡتُ بِرَبِّي وَرَبِّكُم مِّن كُلِّ مُتَكَبِّرٖ لَّا يُؤۡمِنُ بِيَوۡمِ ٱلۡحِسَابِ

Na Mūsā akasema kumwambia Fir'awn na viongozi wa mamlaka yake, «Mimi nimeomba hifadhi kwa Mola wangu na Mola wenu, enyi watu, Anihami na kila mwenye kiburi cha kukataa kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kumtii, asiyeiamini Siku ambayo Mwenyezi Mungu Atawahesabu viumbe Wake.» info
التفاسير:

external-link copy
28 : 40

وَقَالَ رَجُلٞ مُّؤۡمِنٞ مِّنۡ ءَالِ فِرۡعَوۡنَ يَكۡتُمُ إِيمَٰنَهُۥٓ أَتَقۡتُلُونَ رَجُلًا أَن يَقُولَ رَبِّيَ ٱللَّهُ وَقَدۡ جَآءَكُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِ مِن رَّبِّكُمۡۖ وَإِن يَكُ كَٰذِبٗا فَعَلَيۡهِ كَذِبُهُۥۖ وَإِن يَكُ صَادِقٗا يُصِبۡكُم بَعۡضُ ٱلَّذِي يَعِدُكُمۡۖ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهۡدِي مَنۡ هُوَ مُسۡرِفٞ كَذَّابٞ

Na akasema mtu mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu miongoni mwa jamaa za Fir’awn anayeificha Imani yake akiwakemea watu wake, «Vipi nyinyi mtahalalisha kuuawa kwa mtu asiyekuwa na kosa kwenu isipokuwa anasema, ‘Mola wangu ni Mwenyezi Mungu’ na hali yeye amewajia na hoja za yakini kutoka kwa Mola wenu juu ya ukweli wa anayoyasema? Na iwapo Mūsā ni mrongo basi urongo wake utamdhuru mwenyewe, na iwapo ni mkweli basi baadhi ya yale anayowaonya kwayo yatawapata. Hakika Mwenyezi Mungu Hamuelekezi kwenye haki yoyote mwenye kupitisha mpaka kwa kuiacha haki na kuielekea batili, aliye mwingi wa urongo kwa kumnasibishia Mwenyezi Mungu ukiukaji wake. info
التفاسير:

external-link copy
29 : 40

يَٰقَوۡمِ لَكُمُ ٱلۡمُلۡكُ ٱلۡيَوۡمَ ظَٰهِرِينَ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَمَن يَنصُرُنَا مِنۢ بَأۡسِ ٱللَّهِ إِن جَآءَنَاۚ قَالَ فِرۡعَوۡنُ مَآ أُرِيكُمۡ إِلَّا مَآ أَرَىٰ وَمَآ أَهۡدِيكُمۡ إِلَّا سَبِيلَ ٱلرَّشَادِ

«Enyi watu wangu! Utawala ni wenu leo hali ya kuwa mna ushindi katika ardhi ya Misri juu raia wenu miongoni mwa Wana wa Isrāīl na wengineo. Ni nani atakayeizuia adhabu ya Mwenyezi Mungu ikiwa itatushukia?» Fir’awn akasema kuwajibu watu wake, «Siwapatii ushauri, enyi watu, wala mawazo isipokuwa ule ninaouona kuwa ni mzuri na wa sawa kwangu na kwenu. Na siwaiti isipokuwa kwenye njia ya haki na usawa.» info
التفاسير:

external-link copy
30 : 40

وَقَالَ ٱلَّذِيٓ ءَامَنَ يَٰقَوۡمِ إِنِّيٓ أَخَافُ عَلَيۡكُم مِّثۡلَ يَوۡمِ ٱلۡأَحۡزَابِ

Na akasema yule Aliyeamini katika jamaa za Fir’awn kumwambia Fir’awn na viongozi wa mamlaka yake kwa kuwapa ushauri na kuwaonya, «Mimi ninawaogopea mkimuua Mūsā mfano wa siku ya makundi yaliyojikusanya dhidi ya manabii wao. info
التفاسير:

external-link copy
31 : 40

مِثۡلَ دَأۡبِ قَوۡمِ نُوحٖ وَعَادٖ وَثَمُودَ وَٱلَّذِينَ مِنۢ بَعۡدِهِمۡۚ وَمَا ٱللَّهُ يُرِيدُ ظُلۡمٗا لِّلۡعِبَادِ

«Mfano wa mwenendo wa watu wa Nūḥ, 'Ād, Thamūd na waliokuja baada yao katika ukafiri na ukanushaji, ambao Mwenyezi Mungu Aliwaangamiza kwa sababu ya hilo. Na Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika, Hataki kuwafanyia maonevu waja, Akawa Atawaadhibu bila dhambi walilolitenda. Mwenyezi Mungu Yuko juu sana mno kwa kujiepusha na maonevu na upungufu. info
التفاسير:

external-link copy
32 : 40

وَيَٰقَوۡمِ إِنِّيٓ أَخَافُ عَلَيۡكُمۡ يَوۡمَ ٱلتَّنَادِ

«Na enyi watu wangu! Mimi ninawachelea nyinyi adhabu ya Siku ya Kiyama. Siku ambyo wataitana watu wao kwa wao kwa kituko cha Kisimamo Siku hiyo. info
التفاسير:

external-link copy
33 : 40

يَوۡمَ تُوَلُّونَ مُدۡبِرِينَ مَا لَكُم مِّنَ ٱللَّهِ مِنۡ عَاصِمٖۗ وَمَن يُضۡلِلِ ٱللَّهُ فَمَا لَهُۥ مِنۡ هَادٖ

«Siku ambayo mtazunguka muende hali ya kukimbia, hamtakuwa na mwenye kuwahami wala kuwanusuru. Na yoyote yule ambaye Mwenyezi Mungu Atamuachilia Asimuafikie kuufikia uongofu Wake, basi yeye hatakuwa na mtu mwenye kumuongoza kwenye haki na usawa. info
التفاسير: