Traducción de los significados del Sagrado Corán - Traducción al idioma swahili- Abdullah Mohamad y Naser Jamis

Número de página:close

external-link copy
10 : 3

إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَن تُغۡنِيَ عَنۡهُمۡ أَمۡوَٰلُهُمۡ وَلَآ أَوۡلَٰدُهُم مِّنَ ٱللَّهِ شَيۡـٔٗاۖ وَأُوْلَٰٓئِكَ هُمۡ وَقُودُ ٱلنَّارِ

Hakika wale waliokanusha Dini ya haki na wakaikataa, hayatawafaa wao mali yao wala watoto wao kuwaepushia chochote katika adhabu ya Mwenyezi Mungu ikiwashukia ulimwenguni, wala hayatawakinga wao na adhabu Yake Akhera. Na hawa ndio kuni za Moto Siku ya Kiyama. info
التفاسير:

external-link copy
11 : 3

كَدَأۡبِ ءَالِ فِرۡعَوۡنَ وَٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۚ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا فَأَخَذَهُمُ ٱللَّهُ بِذُنُوبِهِمۡۗ وَٱللَّهُ شَدِيدُ ٱلۡعِقَابِ

Hali ya makafiri katika kukanusha kwao na adhabu itakayowashukia ni kama hali ya jamaa za Fir’aun na wale makafiri waliokuwa kabla yao. Wao walizikanusha aya za Mwenyezi Mungu zilizo wazi, Mwenyezi Mungu akawapatiliza kwa kuwatesa kwa sababu ya kukanusha kwao na kushindana. Na Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kutesa kwa aliyemkufuru Yeye na kuwakanusha Mitume Wake. info
التفاسير:

external-link copy
12 : 3

قُل لِّلَّذِينَ كَفَرُواْ سَتُغۡلَبُونَ وَتُحۡشَرُونَ إِلَىٰ جَهَنَّمَۖ وَبِئۡسَ ٱلۡمِهَادُ

Sema, ewe Mtume, kuwaambia makafiri miongoni mwa Mayhudi na wengineo na wale ambao waliudharau ushindi wako katika Badr, «Nyinyi mtashindwa duniani na mtakufa ukafirini, na mtakusanywa mpelekwe kwenye Moto wa Jahanamu, ambao utakuwa ni tandiko la milele kwenu; tandiko baya sana ni hilo.» info
التفاسير:

external-link copy
13 : 3

قَدۡ كَانَ لَكُمۡ ءَايَةٞ فِي فِئَتَيۡنِ ٱلۡتَقَتَاۖ فِئَةٞ تُقَٰتِلُ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ وَأُخۡرَىٰ كَافِرَةٞ يَرَوۡنَهُم مِّثۡلَيۡهِمۡ رَأۡيَ ٱلۡعَيۡنِۚ وَٱللَّهُ يُؤَيِّدُ بِنَصۡرِهِۦ مَن يَشَآءُۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَعِبۡرَةٗ لِّأُوْلِي ٱلۡأَبۡصَٰرِ

Hakika yalikiwa kwenu, enyi Mayahudi wakaidi, ni ushuhuda mkubwa yale mapambano ya Badr yaliyotukia baina ya makundi mawili: kundi moja linapigana kwa ajili ya Dini ya Mwenyezi Mungu, nalo ni kundi la Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na Masahaba wake, na kundi lingine lenye kumkanusha Mwenyezi Mungu, linapigana kwa ajili ya batili. Ukiwatazama Waumini kwa macho utawaona kuwa ni mara mbili ya ile idadi yao. Na Mwenyezi Mungu Alilifanya hilo kuwa ni sababu ya ushindi wa Waislamu juu yao. Na Mwenyezi Mungu Anawasaidia kwa nusura Yake anaowataka katika waja Wake. Hakika katika tukio hili pana mazingatio makubwa kwa wenye busara ambao wanaongokea kujua hukumu zake na matendo Yake. info
التفاسير:

external-link copy
14 : 3

زُيِّنَ لِلنَّاسِ حُبُّ ٱلشَّهَوَٰتِ مِنَ ٱلنِّسَآءِ وَٱلۡبَنِينَ وَٱلۡقَنَٰطِيرِ ٱلۡمُقَنطَرَةِ مِنَ ٱلذَّهَبِ وَٱلۡفِضَّةِ وَٱلۡخَيۡلِ ٱلۡمُسَوَّمَةِ وَٱلۡأَنۡعَٰمِ وَٱلۡحَرۡثِۗ ذَٰلِكَ مَتَٰعُ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَاۖ وَٱللَّهُ عِندَهُۥ حُسۡنُ ٱلۡمَـَٔابِ

Wamepambiwa watu kupenda matamanio ya wanawake na watoto wa kiume na mali mengi ya dhahabu , fedha, farasi wazuri, wanyama wa mifugo miongoni mwa ngamia, ng’ombe na mbuzi na kondoo na ardhi inayotayarishwa kwa kupandwa miti na makulima. Hayo ni mazuri ya uhai wa kilimwengu na pambo lake lenye kutoweka. Na kwa Mwenyezi Mungu kuna marejeo mazuri na thawabu, nayo ni Pepo. info
التفاسير:

external-link copy
15 : 3

۞ قُلۡ أَؤُنَبِّئُكُم بِخَيۡرٖ مِّن ذَٰلِكُمۡۖ لِلَّذِينَ ٱتَّقَوۡاْ عِندَ رَبِّهِمۡ جَنَّٰتٞ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَا وَأَزۡوَٰجٞ مُّطَهَّرَةٞ وَرِضۡوَٰنٞ مِّنَ ٱللَّهِۗ وَٱللَّهُ بَصِيرُۢ بِٱلۡعِبَادِ

Sema ,ewe Mtume, «Je, ni wape habari ya yaliyo bora kuliko yale waliyopambiwa watu katika maisha haya ya kilimwengu? Wale waliomchunga Mwenyezi Mungu na wakaogopa mateso Yake, watakuwa na Pepo ambazo inapita mito chini ya majumba yake ya fahari na miti yake. Watakaa milele humo. Na watakuwa nao humo wake waliotakasika na hedhi na nifasi na tabia mbaya. Na watakuwa na malipo makubwa zaidi kuliko hayo, nayo ni radhi za Mwenyezi Mungu.» Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuchungulia siri za viumbe wake, ni Mjuzi wa hali zao na atawalipa kwa hayo. info
التفاسير: