Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Rowad Translation Center

external-link copy
17 : 2

مَثَلُهُمۡ كَمَثَلِ ٱلَّذِي ٱسۡتَوۡقَدَ نَارٗا فَلَمَّآ أَضَآءَتۡ مَا حَوۡلَهُۥ ذَهَبَ ٱللَّهُ بِنُورِهِمۡ وَتَرَكَهُمۡ فِي ظُلُمَٰتٖ لَّا يُبۡصِرُونَ

Mfano wao ni kama mfano wa aliyekoka moto, na ulipoangaza vile vilivyoko kandokando yake, Mwenyezi Mungu aliiondoa nuru yao na akawaacha katika viza mbalimbali, hawaoni.[1] info

[1] Huu ni mfano wa yule aliyekuwa katika giza kubwa, kwa hivyo akauwasha moto kutoka kwa mtu mwingine. (Tafsir Assa'dii) Na nuru ya moto huo ilitoka kwa Waislamu ambao wao (wanafiki) wanaishi pamoja nao. Na hakusema: Mwenyezi Mungu aliuondoa 'mwangaza wao'. Kwa sababu mwangaza ni ziada juu ya nuru. Kwa hivyo, aliondoa asili (nuru) na ziada yake (mwangaza). (Tafsir Ibn Al-Qayyim)

التفاسير: