Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Rowad Translation Center

external-link copy
135 : 2

وَقَالُواْ كُونُواْ هُودًا أَوۡ نَصَٰرَىٰ تَهۡتَدُواْۗ قُلۡ بَلۡ مِلَّةَ إِبۡرَٰهِـۧمَ حَنِيفٗاۖ وَمَا كَانَ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ

Na wakasema: Kuweni Mayahudi au Wakristo ndio mtaongoka. Sema: Bali tunashika mila ya Ibrahim mwongofu, wala hakuwa katika washirikina.[1] info

[1] Mayahudi na Wakristo huwaita Waislamu kuingia katika Dini zao wakidai kuwa huo ndio uongofu. Lakini Mwenyezi Mungu akakanusha hilo, na kwamba mila (dini) ya Ibrahim ndiyo uongofu. Na katika kuipa mgongo mila yake ni ukafiri na kupotea. (Tafsir Assa'dii)

التفاسير: