Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Rowad Translation Center

Page Number:close

external-link copy
249 : 2

فَلَمَّا فَصَلَ طَالُوتُ بِٱلۡجُنُودِ قَالَ إِنَّ ٱللَّهَ مُبۡتَلِيكُم بِنَهَرٖ فَمَن شَرِبَ مِنۡهُ فَلَيۡسَ مِنِّي وَمَن لَّمۡ يَطۡعَمۡهُ فَإِنَّهُۥ مِنِّيٓ إِلَّا مَنِ ٱغۡتَرَفَ غُرۡفَةَۢ بِيَدِهِۦۚ فَشَرِبُواْ مِنۡهُ إِلَّا قَلِيلٗا مِّنۡهُمۡۚ فَلَمَّا جَاوَزَهُۥ هُوَ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَعَهُۥ قَالُواْ لَا طَاقَةَ لَنَا ٱلۡيَوۡمَ بِجَالُوتَ وَجُنُودِهِۦۚ قَالَ ٱلَّذِينَ يَظُنُّونَ أَنَّهُم مُّلَٰقُواْ ٱللَّهِ كَم مِّن فِئَةٖ قَلِيلَةٍ غَلَبَتۡ فِئَةٗ كَثِيرَةَۢ بِإِذۡنِ ٱللَّهِۗ وَٱللَّهُ مَعَ ٱلصَّٰبِرِينَ

Basi Taluti alipoondoka na majeshi, alisema: Hakika, Mwenyezi Mungu atawajaribu kwa mto. Hivyo basi, atakayekunywa humo, si pamoja nami. Na yule asiyeyaonja, basi huyo atakuwa pamoja nami; ila atakayeteka humo kiasi cha kitanga cha mkono wake. Lakini walikunywa humo isipokuwa wachache tu miongoni mwao. Na alipovuka mto yeye na wale walioamini pamoja naye, walisema: Leo hatumwezi Jaluti (Goliati) na majeshi yake. Wakasema wale wenye yakini ya kukutana na Mwenyezi Mungu: Ni makundi mangapi madogo yalishinda makundi makubwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu? Na Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kusubiri. info
التفاسير:

external-link copy
250 : 2

وَلَمَّا بَرَزُواْ لِجَالُوتَ وَجُنُودِهِۦ قَالُواْ رَبَّنَآ أَفۡرِغۡ عَلَيۡنَا صَبۡرٗا وَثَبِّتۡ أَقۡدَامَنَا وَٱنصُرۡنَا عَلَى ٱلۡقَوۡمِ ٱلۡكَٰفِرِينَ

Na walipotoka ili kupambana na Jaluti na majeshi yake, walisema: Mola wetu Mlezi! Tumiminie subira, na isimamishe imara miguu yetu, na utunusuru kutokana na watu hawa makafiri. info
التفاسير:

external-link copy
251 : 2

فَهَزَمُوهُم بِإِذۡنِ ٱللَّهِ وَقَتَلَ دَاوُۥدُ جَالُوتَ وَءَاتَىٰهُ ٱللَّهُ ٱلۡمُلۡكَ وَٱلۡحِكۡمَةَ وَعَلَّمَهُۥ مِمَّا يَشَآءُۗ وَلَوۡلَا دَفۡعُ ٱللَّهِ ٱلنَّاسَ بَعۡضَهُم بِبَعۡضٖ لَّفَسَدَتِ ٱلۡأَرۡضُ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ ذُو فَضۡلٍ عَلَى ٱلۡعَٰلَمِينَ

Kwa hivyo, wakawashinda kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na Daudi akamuua Jaluti. Na Mwenyezi Mungu akampa Daudi ufalme na hekima, na akamfundisha katika aliyoyataka. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu hawazuii watu kwa watu, basi dunia ingeliharibika. Lakini Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila juu ya walimwengu wote. info
التفاسير:

external-link copy
252 : 2

تِلۡكَ ءَايَٰتُ ٱللَّهِ نَتۡلُوهَا عَلَيۡكَ بِٱلۡحَقِّۚ وَإِنَّكَ لَمِنَ ٱلۡمُرۡسَلِينَ

Hizi ni Aya za Mwenyezi Mungu tunazokusomea kwa haki. Na hakika wewe ni miongoni mwa Mitume. info
التفاسير: