Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Rowad Translation Center

Page Number:close

external-link copy
89 : 10

قَالَ قَدۡ أُجِيبَت دَّعۡوَتُكُمَا فَٱسۡتَقِيمَا وَلَا تَتَّبِعَآنِّ سَبِيلَ ٱلَّذِينَ لَا يَعۡلَمُونَ

Mwenyezi Mungu akasema: Hakika maombi yenu wawili yameshakubaliwa. Basi nyookeni, wala msifuate njia ya wale wasiojua. info
التفاسير:

external-link copy
90 : 10

۞ وَجَٰوَزۡنَا بِبَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ ٱلۡبَحۡرَ فَأَتۡبَعَهُمۡ فِرۡعَوۡنُ وَجُنُودُهُۥ بَغۡيٗا وَعَدۡوًاۖ حَتَّىٰٓ إِذَآ أَدۡرَكَهُ ٱلۡغَرَقُ قَالَ ءَامَنتُ أَنَّهُۥ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا ٱلَّذِيٓ ءَامَنَتۡ بِهِۦ بَنُوٓاْ إِسۡرَٰٓءِيلَ وَأَنَا۠ مِنَ ٱلۡمُسۡلِمِينَ

Tukawavusha bahari Wana wa Israili, naye Firauni na askari wake wakawafuata kwa dhuluma na uadui. Mpaka kuzama kulipomfikia, akasema: Nimeamini kuwa hakuna mungu isipokuwa yule ambaye walimwamini Wana wa Israili, na mimi ni miongoni mwa Waislamu. info
التفاسير:

external-link copy
91 : 10

ءَآلۡـَٰٔنَ وَقَدۡ عَصَيۡتَ قَبۡلُ وَكُنتَ مِنَ ٱلۡمُفۡسِدِينَ

Je, sasa? Na ilhali uliasi kabla yake na ukawa miongoni mwa waharibifu? info
التفاسير:

external-link copy
92 : 10

فَٱلۡيَوۡمَ نُنَجِّيكَ بِبَدَنِكَ لِتَكُونَ لِمَنۡ خَلۡفَكَ ءَايَةٗۚ وَإِنَّ كَثِيرٗا مِّنَ ٱلنَّاسِ عَنۡ ءَايَٰتِنَا لَغَٰفِلُونَ

Leo basi, tutakuokoa kwa mwili wako, ili uwe Ishara kwa wale walio nyuma yako. Na hakika watu wengi wameghafilika mbali na Ishara zetu. info
التفاسير:

external-link copy
93 : 10

وَلَقَدۡ بَوَّأۡنَا بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ مُبَوَّأَ صِدۡقٖ وَرَزَقۡنَٰهُم مِّنَ ٱلطَّيِّبَٰتِ فَمَا ٱخۡتَلَفُواْ حَتَّىٰ جَآءَهُمُ ٱلۡعِلۡمُۚ إِنَّ رَبَّكَ يَقۡضِي بَيۡنَهُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ فِيمَا كَانُواْ فِيهِ يَخۡتَلِفُونَ

Na hakika tuliwaandalia Wana wa Israili makao mema, na tukawaruzuku katika vitu vizuri. Nao hawakuhitilafiana mpaka ilipowafikia elimu. Hakika Mola wako Mlezi atahukumu baina yao Siku ya Kiyama katika yale waliyokuwa wakihitilafiana. info
التفاسير:

external-link copy
94 : 10

فَإِن كُنتَ فِي شَكّٖ مِّمَّآ أَنزَلۡنَآ إِلَيۡكَ فَسۡـَٔلِ ٱلَّذِينَ يَقۡرَءُونَ ٱلۡكِتَٰبَ مِن قَبۡلِكَۚ لَقَدۡ جَآءَكَ ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّكَ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡمُمۡتَرِينَ

Na ikiwa uko katika shaka juu ya yale tuliyokuteremshia, basi waulize wale wasomao Kitabu kabla yako. Kwa yakini imekwishakujia haki kutoka kwa Mola wako Mlezi. Basi kamwe usiwe miongoni mwa wenye shaka. info
التفاسير:

external-link copy
95 : 10

وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ فَتَكُونَ مِنَ ٱلۡخَٰسِرِينَ

Na kamwe usiwe miongoni mwa wale waliozikadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu, ukawa katika waliohasiri. info
التفاسير:

external-link copy
96 : 10

إِنَّ ٱلَّذِينَ حَقَّتۡ عَلَيۡهِمۡ كَلِمَتُ رَبِّكَ لَا يُؤۡمِنُونَ

Hakika wale ambao neno la Mola wako Mlezi limekwishathibitika juu yao, hawataamini. info
التفاسير:

external-link copy
97 : 10

وَلَوۡ جَآءَتۡهُمۡ كُلُّ ءَايَةٍ حَتَّىٰ يَرَوُاْ ٱلۡعَذَابَ ٱلۡأَلِيمَ

Hata kama itawajia kila Ishara, mpaka waione adhabu chungu. info
التفاسير: