Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Rowad Translation Center

Al-Fatihah

external-link copy
1 : 1

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 1

ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu.[1] info

[1] Mola Mlezi ni yule anayewalea walimwengu wote. Nao walimwengu ni kila kisichokuwa Mwenyezi Mungu.

التفاسير:

external-link copy
3 : 1

ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.[1] info

[1] Katika misingi waliyokubaliana juu yake watangulizi wema wa umma huu na maimamu wake ni kuamini kwamba Mwenyezi Mungu ana majina na sifa nzuri nzuri.

التفاسير:

external-link copy
4 : 1

مَٰلِكِ يَوۡمِ ٱلدِّينِ

Mmiliki wa Siku ya Malipo. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 1

إِيَّاكَ نَعۡبُدُ وَإِيَّاكَ نَسۡتَعِينُ

Ni Wewe tu tunayeabudu, na ni Wewe tu tunayeomba msaada. info
التفاسير:

external-link copy
6 : 1

ٱهۡدِنَا ٱلصِّرَٰطَ ٱلۡمُسۡتَقِيمَ

Tuongoe kwenye njia iliyonyooka. info
التفاسير:

external-link copy
7 : 1

صِرَٰطَ ٱلَّذِينَ أَنۡعَمۡتَ عَلَيۡهِمۡ غَيۡرِ ٱلۡمَغۡضُوبِ عَلَيۡهِمۡ وَلَا ٱلضَّآلِّينَ

Njia ya wale uliowaneemesha. Siyo ya wale waliokasirikiwa, wala waliopotea. info
التفاسير: