Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Ali Muhsen Al-Berwani

external-link copy
127 : 9

وَإِذَا مَآ أُنزِلَتۡ سُورَةٞ نَّظَرَ بَعۡضُهُمۡ إِلَىٰ بَعۡضٍ هَلۡ يَرَىٰكُم مِّنۡ أَحَدٖ ثُمَّ ٱنصَرَفُواْۚ صَرَفَ ٱللَّهُ قُلُوبَهُم بِأَنَّهُمۡ قَوۡمٞ لَّا يَفۡقَهُونَ

Na ikiteremka Sura hutazamana wao kwa wao, (kama kwamba wanasema:) Je! Yuko mtu anakuoneni? Kisha hugeukilia mbali. Mwenyezi amezigeuza nyoyo zao kwa kuwa hao ni watu wasio fahamu. info

Na kadhaalika ikiteremka Sura nao wapo barazani kwa Mtume hukonyezana na kuambiana: Yuko mtu anaye kuoneni? Tena nyoyo zao hukengeuka wasimfuate Mtume wala wasimuamini! Mwenyezi Mungu amewazidisha kupotea kwa vile kushikilia kwao kubaki katika upotovu na kuikataa Haki, kwani watu hawa hawafahamu kitu!

التفاسير: