Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Ali Muhsen Al-Berwani

Al-Falaq

external-link copy
1 : 113

قُلۡ أَعُوذُ بِرَبِّ ٱلۡفَلَقِ

Sema: Najikinga kwa Mola Mlezi wa mapambazuko, info

Sema najikinga na Mola Mlezi wa asubuhi inapo pambazuka kutokana na usiku.

التفاسير:

external-link copy
2 : 113

مِن شَرِّ مَا خَلَقَ

Na shari ya alivyo viumba, info

Na shari ya kila chenye shari katika viumbe, ambavyo hapana wa kuzuia shari yao ila Mwenye kumiliki amri yao.

التفاسير:

external-link copy
3 : 113

وَمِن شَرِّ غَاسِقٍ إِذَا وَقَبَ

Na shari ya giza la usiku liingiapo, info

Na shari ya usiku unapo kuwa totoro.

التفاسير:

external-link copy
4 : 113

وَمِن شَرِّ ٱلنَّفَّٰثَٰتِ فِي ٱلۡعُقَدِ

Na shari ya wanao pulizia mafundoni, info

Na shari ya anaye pita baina ya watu kwa sababu ya kuwafisidi.

التفاسير:

external-link copy
5 : 113

وَمِن شَرِّ حَاسِدٍ إِذَا حَسَدَ

Na shari ya hasidi anapo husudu. info

Na shari ya hasidi anaye tamani iondoke neema kwa wengine.

التفاسير: