Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis

Al-Qadr

external-link copy
1 : 97

إِنَّآ أَنزَلۡنَٰهُ فِي لَيۡلَةِ ٱلۡقَدۡرِ

Sisi Tumeiteremsha Qur’ani katika usiku wa cheo na utukufu , nao ni moja wa masiku ya mwezi wa Ramdhani. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 97

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا لَيۡلَةُ ٱلۡقَدۡرِ

Na nilipi liliokujulisha, ewe Mtume, ni upi usiku wa cheo na utukufu? info
التفاسير:

external-link copy
3 : 97

لَيۡلَةُ ٱلۡقَدۡرِ خَيۡرٞ مِّنۡ أَلۡفِ شَهۡرٖ

Usiku wa cheo na utukufu ni bora fadhila zake kuliko fadhila za miezi elfu moja isiyokuwa usiku huo. info
التفاسير:

external-link copy
4 : 97

تَنَزَّلُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ وَٱلرُّوحُ فِيهَا بِإِذۡنِ رَبِّهِم مِّن كُلِّ أَمۡرٖ

Usiku huo hushuka Malaika na Jibrili, amani iwashukie, kwa ruhusa ya Mola wao kwa kila jambo Alilolikadiria liwe mwaka huo. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 97

سَلَٰمٌ هِيَ حَتَّىٰ مَطۡلَعِ ٱلۡفَجۡرِ

Usiku huo wote ni amani, hakuna shari, mpaka kutokea alfajiri. info
التفاسير: