Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis

external-link copy
117 : 7

۞ وَأَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰ مُوسَىٰٓ أَنۡ أَلۡقِ عَصَاكَۖ فَإِذَا هِيَ تَلۡقَفُ مَا يَأۡفِكُونَ

Hapo Mwenyezi Mungu Alimletea wahyi mja Wake na Mtume Wake Mūsā, amani imshukiye, katika kisimamo hicho kikubwa ambacho hapo Mwenyezi Mungu Alipambanua baina ya ukweli na urongo, akimuamuru akitupe kilichoko kwenye mkono wake wa kulia, nacho ni fimbo yake. Akaitupa na papo hapo ikawa inavimeza vile wanavyovitupa na kuwafanya watu wadhanie kuwa ni vya kweli na ilhali ni vya urongo. info
التفاسير: