Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis

external-link copy
3 : 6

وَهُوَ ٱللَّهُ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَفِي ٱلۡأَرۡضِ يَعۡلَمُ سِرَّكُمۡ وَجَهۡرَكُمۡ وَيَعۡلَمُ مَا تَكۡسِبُونَ

Na Mwenyezi Mungu, Aliyetakata na kila sifa ya upungufu, Ndiye Mola Mwenye kuabudiwa kwa haki mbinguni na ardhini. Na miongoni mwa dalili za uungu wake ni kwamba Yeye Anayajua yote mnayoyaficha, enyi watu, na mnayoyadhihirisha na Anayajua matendo yenu yote, mazuri na mabaya. Na kwa ajili hii, Yeye Peke Yake, Aliyetukuka na kuwa juu, Ndiye Mola Anayestahiki kuabudiwa. info
التفاسير: