Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis

Page Number:close

external-link copy
138 : 6

وَقَالُواْ هَٰذِهِۦٓ أَنۡعَٰمٞ وَحَرۡثٌ حِجۡرٞ لَّا يَطۡعَمُهَآ إِلَّا مَن نَّشَآءُ بِزَعۡمِهِمۡ وَأَنۡعَٰمٌ حُرِّمَتۡ ظُهُورُهَا وَأَنۡعَٰمٞ لَّا يَذۡكُرُونَ ٱسۡمَ ٱللَّهِ عَلَيۡهَا ٱفۡتِرَآءً عَلَيۡهِۚ سَيَجۡزِيهِم بِمَا كَانُواْ يَفۡتَرُونَ

Na walisema washirikina kwamba ngamia hawa na makulima haya ni vitu haramu; haifai kuvila kwa mtu yoyote isipokuwa yule wanayemruhusu, kulingana na madai yao, miongoni mwa wasimamizi wa mizimu na wengineo. Na hawa ni ngamia ambao ilipewa heshima migongo yao, haifai kupandwa wala kubebeshwa vitu juu yake kwa namana yoyote. Na hawa ni ngamia ambao hawawatajii jina la Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, katika jambo lolote linalowahusu wao.Waliyafanya hayo kwa urongo utokao kwao, kumzulia Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu Atawalipa kwa urongo waliokuwa wakimzulia Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake. info
التفاسير:

external-link copy
139 : 6

وَقَالُواْ مَا فِي بُطُونِ هَٰذِهِ ٱلۡأَنۡعَٰمِ خَالِصَةٞ لِّذُكُورِنَا وَمُحَرَّمٌ عَلَىٰٓ أَزۡوَٰجِنَاۖ وَإِن يَكُن مَّيۡتَةٗ فَهُمۡ فِيهِ شُرَكَآءُۚ سَيَجۡزِيهِمۡ وَصۡفَهُمۡۚ إِنَّهُۥ حَكِيمٌ عَلِيمٞ

Na walisema washirikina, «Watoto waliyomo ndani ya wanyama howa, wakizaliwa wakiwa hai, ni halali tu kwa wanaume kati yetu na ni haramu kwa wanawake miongoni mwetu.» Na wakizaliwa nao wamekufa wanashirikiana katika kuwatumia. Mwenyezi Mungu Atawatesa kwa kujiwekea sheria za kuhalalisha na kuharamisha ambazo Mwenyezi Mungu hakuziruhusu. Hakika Yeye Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, ni Mwingi wa hekima katika uendeshaji Wake mambo ya viumbe Wake, Mjuzi sana kuhusu wao. info
التفاسير:

external-link copy
140 : 6

قَدۡ خَسِرَ ٱلَّذِينَ قَتَلُوٓاْ أَوۡلَٰدَهُمۡ سَفَهَۢا بِغَيۡرِ عِلۡمٖ وَحَرَّمُواْ مَا رَزَقَهُمُ ٱللَّهُ ٱفۡتِرَآءً عَلَى ٱللَّهِۚ قَدۡ ضَلُّواْ وَمَا كَانُواْ مُهۡتَدِينَ

Hakika wamepata hasara na wameangamia wale ambao, kwa udhaifu wa akili zao na kwa ujinga wao, waliwaua watoto wao na wakaziharamisha, kwa kumzulia Mwenyezi Mungu urongo, zile Alizowaruzuku. Wako mabali na haki na hawakuwa ni miongoni mwa watu wa uongofu na muelekeo wa sawa. Kuhalalisha na kuharamisha ni miongoni mwa mambo mahususi ya uungu katika uwekaji sheria. Halali ni Aliyoihalalisha Mwenyezi Mungu, na haramu ni Aliyoiharamisha Mwenyezi Mungu. Na haipasii kwa yoyote kati ya viumbe wake, awe mmoja au kundi, kuwaekea sheria waja Wake ambayo Mwenyezi Mungu Hakuidhinisha. info
التفاسير:

external-link copy
141 : 6

۞ وَهُوَ ٱلَّذِيٓ أَنشَأَ جَنَّٰتٖ مَّعۡرُوشَٰتٖ وَغَيۡرَ مَعۡرُوشَٰتٖ وَٱلنَّخۡلَ وَٱلزَّرۡعَ مُخۡتَلِفًا أُكُلُهُۥ وَٱلزَّيۡتُونَ وَٱلرُّمَّانَ مُتَشَٰبِهٗا وَغَيۡرَ مُتَشَٰبِهٖۚ كُلُواْ مِن ثَمَرِهِۦٓ إِذَآ أَثۡمَرَ وَءَاتُواْ حَقَّهُۥ يَوۡمَ حَصَادِهِۦۖ وَلَا تُسۡرِفُوٓاْۚ إِنَّهُۥ لَا يُحِبُّ ٱلۡمُسۡرِفِينَ

Na Mwenyezi Mungu, kutkata na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, Ndiye Aliyewaanzishia mashamba: miongoni mwa mimea yake kuna ile iliyoinuliwa juu ya ardhi na kuegemezewa vitu vyingine, kama mizabibu, na miongoni mwayo kuna isiyoinuliwa, bali inasimama yenyewe kwenye vigogo vyake, kama mitende na miti mingine ya mazao. Mimea yote hiyo ikiwa ina tamu tafauti. Mizabibu na mikomamanga, maumbile yake yanafanana na matunda yake yanatafautiana tamu yake. Kuleni, enyi watu, matunda yake na mtoe Zaka zake zilizolazimishwa kwenu siku mnapoyavuna na kuyatungua, na msiikiuke mipaka ya usawa katika kutoa mali na kula chakula na mengineyo. Hakika Yeye, Mwenyezi Mungu, Hawapendi wenye kukiuka mipaka Yake kwa kutumia mali katika njia zisokuwa zake. info
التفاسير:

external-link copy
142 : 6

وَمِنَ ٱلۡأَنۡعَٰمِ حَمُولَةٗ وَفَرۡشٗاۚ كُلُواْ مِمَّا رَزَقَكُمُ ٱللَّهُ وَلَا تَتَّبِعُواْ خُطُوَٰتِ ٱلشَّيۡطَٰنِۚ إِنَّهُۥ لَكُمۡ عَدُوّٞ مُّبِينٞ

Na Ameleta katika wanyama wale ambao wametayarishwa kwa kubebeshwa kwa kuwa ni wakubwa na ni warefu, kama ngamia. Na miongoni mwao kuna waliotayarishwa si kwa kubebeshwa kwa kuwa ni wadogo na wafupi, kama ng’ombe, mbuzi na kondoo. Kuleni wale Aliyowahalalishia nyinyi Mwenyezi Mungu miongoni mwa hawa wanyama, wala msiwaharamishe wale Aliyowahalalisha miongoni mwao kwa kufuata njia za Shetani kama walivyofanya washirikina. Hakika Shetani, kwenu nyinyi, ni adui mwenye uadui wa wazi. info
التفاسير: