Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis

external-link copy
38 : 5

وَٱلسَّارِقُ وَٱلسَّارِقَةُ فَٱقۡطَعُوٓاْ أَيۡدِيَهُمَا جَزَآءَۢ بِمَا كَسَبَا نَكَٰلٗا مِّنَ ٱللَّهِۗ وَٱللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٞ

Na mwizi wa kiume na mwizi wa kike, wakateni, enyi watawala, mikono yao kuambatana na Sheria. Hayo yakiwa ni malipo yao kwa kuchukua kwao mali ya watu pasi na haki, na ni mateso ambayo kwayo Mwenyezi Mungu Anawazuia wengineo kufanya mfano wa kitendo chao. Na Mwenyezi Mungu ni Mshindi katika mamlaka Yake, ni Mwenye hekima katika amri Zake na makatazo Yake. info
التفاسير: