Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis

external-link copy
31 : 4

إِن تَجۡتَنِبُواْ كَبَآئِرَ مَا تُنۡهَوۡنَ عَنۡهُ نُكَفِّرۡ عَنكُمۡ سَيِّـَٔاتِكُمۡ وَنُدۡخِلۡكُم مُّدۡخَلٗا كَرِيمٗا

Mkijiepusha, enyi Waumini, na madhambi makubwa, kama kumshrikisha Mwenyezi Mungu, kuwaasi wazazi wawili, kumuua mtu bila ya haki na mengineyo, tutawasamehe madhambi yenu madogo yaliyo chini ya hayo na tutawaingiza mahali pema pa kuingia, napo ni Pepo. info
التفاسير: