Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis

Page Number:close

external-link copy
23 : 34

وَلَا تَنفَعُ ٱلشَّفَٰعَةُ عِندَهُۥٓ إِلَّا لِمَنۡ أَذِنَ لَهُۥۚ حَتَّىٰٓ إِذَا فُزِّعَ عَن قُلُوبِهِمۡ قَالُواْ مَاذَا قَالَ رَبُّكُمۡۖ قَالُواْ ٱلۡحَقَّۖ وَهُوَ ٱلۡعَلِيُّ ٱلۡكَبِيرُ

Na maombezi ya mwenye kuombea hayafal kitu hayanufaishi mbele Yake, isipokuwa kwa yule Aliyemruhusu. Na miongoni mwa utukufu Wake na utisho Wake, Aliyeshinda na kutukuka, ni kuwa Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, Anapotamka wahyi na watu wa mbinguni wakayasikia maneno Yake, wanakuwa katika hali ya kutetemeka kwa utisho, mpaka wanakuwa katika hali kama ile ya kukosa fahamu. Na kibabaiko kinapowaondokea kwenye nyoyo zao wanaulizana wao kwa wao, «Amesema nini Mola wenu?» Malaika watasema, «Amesema kweli! Na Yeye Yuko juu kwa dhati Yake, utendaji nguvu Wake na utukufu wa cheo Chake, Aliye Mkubwa juu ya kila kitu.» info
التفاسير:

external-link copy
24 : 34

۞ قُلۡ مَن يَرۡزُقُكُم مِّنَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ قُلِ ٱللَّهُۖ وَإِنَّآ أَوۡ إِيَّاكُمۡ لَعَلَىٰ هُدًى أَوۡ فِي ضَلَٰلٖ مُّبِينٖ

Sema, ewe Mtume, kuwaambia washirikina, «Ni nani anayewaruzuku kwa mvua kutoka mbinguni, na kwa mimea na madini na vinginevyo kutoka ardhini?» Hivyo basi hawana budi kukubali kuwa Yeye ni Mwenyezi Mungu. Na iwapo hawatakubali hilo, waambie, «Mwenyezi Mungu Ndiye Mwingi wa kuruzuku, na kwa hakika mojawapo wa mapote mawili, kati ya sisi na nyinyi, limejikita kwenye uongofu au limevama kwenye upotevu ulio wazi.» info
التفاسير:

external-link copy
25 : 34

قُل لَّا تُسۡـَٔلُونَ عَمَّآ أَجۡرَمۡنَا وَلَا نُسۡـَٔلُ عَمَّا تَعۡمَلُونَ

Sema, «Hamtaulizwa kuhusu dhambi zetu, wala hatutaulizwa kuhusu matendo yenu, sababu sisi tumejitenga na nyinyi na ukanushaji wenu.» info
التفاسير:

external-link copy
26 : 34

قُلۡ يَجۡمَعُ بَيۡنَنَا رَبُّنَا ثُمَّ يَفۡتَحُ بَيۡنَنَا بِٱلۡحَقِّ وَهُوَ ٱلۡفَتَّاحُ ٱلۡعَلِيمُ

Sema, «Mola wetu Atatukusanya baina yetu na nyinyi Siku ya Kiyama, kisha Atatoa uamuzi wa uadilifu baina yetu. Na Yeye Ndiye Mfunguzi Mwenye kutoa uamuzi baina ya viumbe Vyake, Mwingi wa ujuzi wa yale yanayotakikana yatolewe uamuzi na hali ya viumbe Vyake. Hakuna kinachofichicana Kwake chochote.» info
التفاسير:

external-link copy
27 : 34

قُلۡ أَرُونِيَ ٱلَّذِينَ أَلۡحَقۡتُم بِهِۦ شُرَكَآءَۖ كَلَّاۚ بَلۡ هُوَ ٱللَّهُ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ

Sema, «Nionesheni kwa hoja na dalili wale mliomshikanisha na Mwenyezi Mungu mkawafanya ni washirika Wake katika kuabudiwa, je wao wameumba chochote? Mambo si kama walivyoeleza.Bali Yeye Ndiye Mwenye kuabudiwa kwa haki, ambaye hana mshirika wake, aliye Mshindi katika kuwatesa waliomshirikisha, na mwenye hekima katika maneno Yake, vitendo Vyake na upelekeshaji mambo ya viumbe Vyake. info
التفاسير:

external-link copy
28 : 34

وَمَآ أَرۡسَلۡنَٰكَ إِلَّا كَآفَّةٗ لِّلنَّاسِ بَشِيرٗا وَنَذِيرٗا وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعۡلَمُونَ

Na hatukukutumiliza, ewe Mtume, isipokuwa ni kwa watu wote, uwabashirie malipo mema ya Mwenyezi Mungu na uwaonye mateso Yake. Lakini wengi wa watu hawaijui haki, hivyo basi wao wanaipa mgongo. info
التفاسير:

external-link copy
29 : 34

وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَٰذَا ٱلۡوَعۡدُ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Na hawa washirikina wanasema kwa njia ya shere, «Ni lini wakati wa Ahadi hii ambayo unatuahidi kuwa Mwenyezi Mungu Atatukusanya ndani yake kisha Ahukumu baina yetu, iwapo nyinyi ni wakweli katika kile mlichotuahidi kwacho?» info
التفاسير:

external-link copy
30 : 34

قُل لَّكُم مِّيعَادُ يَوۡمٖ لَّا تَسۡتَـٔۡخِرُونَ عَنۡهُ سَاعَةٗ وَلَا تَسۡتَقۡدِمُونَ

Waamnbie, ewe Mtume, «Nyinyi muna maagano ambayo hapana budi yatawajia, nayo ni maagano ya Siku ya Kiyama, hamtachelewa nayo hata muda mchache wa kupata kutubia, na wala hamtatangulia mbele yake mkaadhibiwa hata kwa muda mchache. Basi jihadharini na Siku hiyo na jitayarisheni kwa vifaa vyake.» info
التفاسير:

external-link copy
31 : 34

وَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَن نُّؤۡمِنَ بِهَٰذَا ٱلۡقُرۡءَانِ وَلَا بِٱلَّذِي بَيۡنَ يَدَيۡهِۗ وَلَوۡ تَرَىٰٓ إِذِ ٱلظَّٰلِمُونَ مَوۡقُوفُونَ عِندَ رَبِّهِمۡ يَرۡجِعُ بَعۡضُهُمۡ إِلَىٰ بَعۡضٍ ٱلۡقَوۡلَ يَقُولُ ٱلَّذِينَ ٱسۡتُضۡعِفُواْ لِلَّذِينَ ٱسۡتَكۡبَرُواْ لَوۡلَآ أَنتُمۡ لَكُنَّا مُؤۡمِنِينَ

Na waliokanusha walisema, «Hatutaiamini hii Qur’ani wala vile vilivyoitangulia, kina Taurati, Injili na Zaburi.» Kwa hakika washakanusha vitabu vyote vya Mwenyezi Mungu. Na lau utaona pindi madhalimu wamefungwa mbele ya Mola wao ili wahesabiwe, huku wakirudishiana maneno baina yao, kila mmoja anamtupia lawama mwingine, utaona jambo la kutisha! Watakuwa waliokuwa wakifanywa wanyonge wakisema kuwaambia wale waliokuwa na kiburi, nao ni wale viongozi na wakubwa waliopotea na kupoteza, «Lau si nyinyi kutupoteza njia tungalikuwa ni wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake.» info
التفاسير: