Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis

Page Number:close

external-link copy
33 : 25

وَلَا يَأۡتُونَكَ بِمَثَلٍ إِلَّا جِئۡنَٰكَ بِٱلۡحَقِّ وَأَحۡسَنَ تَفۡسِيرًا

Na hawakujii, ewe Mtume, hawa washirikina na hoja yoyote au utata wowote isipokuwa tutakuletea majibu ya ukweli na ufafanuzi wake mzuri zaidi. info
التفاسير:

external-link copy
34 : 25

ٱلَّذِينَ يُحۡشَرُونَ عَلَىٰ وُجُوهِهِمۡ إِلَىٰ جَهَنَّمَ أُوْلَٰٓئِكَ شَرّٞ مَّكَانٗا وَأَضَلُّ سَبِيلٗا

Hao makafiri ndio watakaoburutwa kwa nyuso zao hadi kwenye Moto wa Jahanamu. Hao ndio wenye mashukio mabaya kabisa miongoni mwa watu na ndio walioko mbali kabisa na njia ya haki. info
التفاسير:

external-link copy
35 : 25

وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَا مُوسَى ٱلۡكِتَٰبَ وَجَعَلۡنَا مَعَهُۥٓ أَخَاهُ هَٰرُونَ وَزِيرٗا

Na kwa hakika, tulimpelekea Mūsā Taurati, tukamfanya ndugu yake Hārūn kuwa ni msaidizi wake info
التفاسير:

external-link copy
36 : 25

فَقُلۡنَا ٱذۡهَبَآ إِلَى ٱلۡقَوۡمِ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا فَدَمَّرۡنَٰهُمۡ تَدۡمِيرٗا

na tukawaambia wao wawili,»Endeni kwa Fir’awn na watu wake waliozikanusha dalili za uola[7] wetu na uungu wetu.» Basi wakawaendea na wakawalingania wamuamini Mwenyezi Mungu, wamtii na wasimshirikishe. Wakawakanusha, na kwa hivyo tukawaangamiza maangamivu makubwa. info

[7]Dalili ya uola wa Mwenyezi Mungu ni dalili ya kuwa yeye Ndiye Mola

التفاسير:

external-link copy
37 : 25

وَقَوۡمَ نُوحٖ لَّمَّا كَذَّبُواْ ٱلرُّسُلَ أَغۡرَقۡنَٰهُمۡ وَجَعَلۡنَٰهُمۡ لِلنَّاسِ ءَايَةٗۖ وَأَعۡتَدۡنَا لِلظَّٰلِمِينَ عَذَابًا أَلِيمٗا

Na tuliwazamisha watu wa Nūḥ kwa mafuriko walipomkanusha. Na mwenye kumkanusha Mtume yoyote huwa amewakanusha Mitume wote. Na tulikufanya kule kuwazamisha ni mazingatio kwa watu. Na tutawapatia wao na wale waliofuata njia yao katika kukanusha, Siku ya Kiyama, adhabu yenye kuumiza. info
التفاسير:

external-link copy
38 : 25

وَعَادٗا وَثَمُودَاْ وَأَصۡحَٰبَ ٱلرَّسِّ وَقُرُونَۢا بَيۡنَ ذَٰلِكَ كَثِيرٗا

Na tuliwaangamiza hao ‘Ād, watu wa Hūd, na Thamūd, watu wa Ṣāliḥ, na watu wa Kisimani na watu wengine wengi waliokuwako baina ya watu wa Nūḥ, kina ‘Ād, kina Thamūd na watu wa Rass(hapo kisimani) hakuna awajuao isipokuwa Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
39 : 25

وَكُلّٗا ضَرَبۡنَا لَهُ ٱلۡأَمۡثَٰلَۖ وَكُلّٗا تَبَّرۡنَا تَتۡبِيرٗا

Na ummah wote hao tuliwabainishia hoja na kuwafafanulia dalili na tukawaondolea nyudhuru (za kutojua). Pamoja na hivyo, hawakuamini, na kwa ajili hiyo tuliwapa maangamivu kwa kuwaadhibu. info
التفاسير:

external-link copy
40 : 25

وَلَقَدۡ أَتَوۡاْ عَلَى ٱلۡقَرۡيَةِ ٱلَّتِيٓ أُمۡطِرَتۡ مَطَرَ ٱلسَّوۡءِۚ أَفَلَمۡ يَكُونُواْ يَرَوۡنَهَاۚ بَلۡ كَانُواْ لَا يَرۡجُونَ نُشُورٗا

Na washirikina wa Makkah walikuwa wakikipitia kijiji cha watu wa Lūṭ katika safari zao, nacho ni kijiji cha Sadūm ambacho kiliangamizwa kwa mawe kutoka mbinguni, wasizingatie kwa hilo, bali walikuwa hawatazamii kuwa kuna marejeo Siku ya Kiyama ambapo wao watalipwa. info
التفاسير:

external-link copy
41 : 25

وَإِذَا رَأَوۡكَ إِن يَتَّخِذُونَكَ إِلَّا هُزُوًا أَهَٰذَا ٱلَّذِي بَعَثَ ٱللَّهُ رَسُولًا

Na wakuonapo hao wakanushaji, ewe Mtume, wanakufanyia shere wakisema, «Je, ni huyu yule anayedai kwamba Mwenyezi Mungu Amemtumiliza kuwa ni mjumbe kwetu? info
التفاسير:

external-link copy
42 : 25

إِن كَادَ لَيُضِلُّنَا عَنۡ ءَالِهَتِنَا لَوۡلَآ أَن صَبَرۡنَا عَلَيۡهَاۚ وَسَوۡفَ يَعۡلَمُونَ حِينَ يَرَوۡنَ ٱلۡعَذَابَ مَنۡ أَضَلُّ سَبِيلًا

Yeye amekaribia kutuepusha na kuwaabudu masanamu wetu kwa hoja zake za nguvu na ufasaha wake, lau hatungalisimama imara juu ya kuwaabudu.» Na watajuwa, watakapoiona adhabu wanayoistahili, ni nani aliyepotoka zaidi kidini: ni wao au ni Muhammad? info
التفاسير:

external-link copy
43 : 25

أَرَءَيۡتَ مَنِ ٱتَّخَذَ إِلَٰهَهُۥ هَوَىٰهُ أَفَأَنتَ تَكُونُ عَلَيۡهِ وَكِيلًا

Mwangalie, ewe Mtume, kwa kumuonea ajabu yule aliyeyatii matamanio yake kama kumtii Mwenyezi Mungu. Je, wewe utakuwa ni mwenye kumtunza mpaka umrudishe kwenye Imani? info
التفاسير: