Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis

external-link copy
29 : 22

ثُمَّ لۡيَقۡضُواْ تَفَثَهُمۡ وَلۡيُوفُواْ نُذُورَهُمۡ وَلۡيَطَّوَّفُواْ بِٱلۡبَيۡتِ ٱلۡعَتِيقِ

Kisha wale mahujaji wakamilishe matendo ya ibada yaliyosalia ya kujifungua na kutoka kwenye kifungo cha ibada yao ya Hija, nako ni kwa kuondoa uchafu uliokusanyika kwenye miili yao, kukata kucha zao na kunyoa nywele zao, na watekeleze yale waliyojilazimsha nafsi zao ya kuhiji na kufanya Umra na kuchinja wanyama wa tunu, na waitufu kwa kuizunguka Nyumba huru ya kale ambayo Mwenyezi Mungu Ameikomboa isitawaliwe kimabavu na watu wasioijali, nayo ni Alkaba. info
التفاسير: