Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis

external-link copy
82 : 2

وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ أُوْلَٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡجَنَّةِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ

Na hukumu ya Mwenyezi Mungu iliyothibiti, kwa upande mwengine, ni kwamba wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mitume Wake imani ya kikweli iliyosafika na Wakafanya vitendo vinavyoambatana na Sheria ya Mwenyezi Mungu Aliyowapelekea Mitume Wake kwa njia ya Wahyi, hao watakaa Peponi makao ya milele yasiyokatika huko Akhera. info
التفاسير: