Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis

external-link copy
81 : 2

بَلَىٰۚ مَن كَسَبَ سَيِّئَةٗ وَأَحَٰطَتۡ بِهِۦ خَطِيٓـَٔتُهُۥ فَأُوْلَٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ

Hukumu ya Mwenyezi Mungu imethibiti kwamba mwenye kutenda makosa mpaka yakamtia ukafirini na madhambi yake yakamtawala yeye sehemu zake zote, na hali hii haiwi isipokuwa kwa mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu, wote hao, washirikina na makafiri, ndio wenye kukaa Motoni makao ya milele yasiyokatika. info
التفاسير: