Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis

Page Number:close

external-link copy
16 : 18

وَإِذِ ٱعۡتَزَلۡتُمُوهُمۡ وَمَا يَعۡبُدُونَ إِلَّا ٱللَّهَ فَأۡوُۥٓاْ إِلَى ٱلۡكَهۡفِ يَنشُرۡ لَكُمۡ رَبُّكُم مِّن رَّحۡمَتِهِۦ وَيُهَيِّئۡ لَكُم مِّنۡ أَمۡرِكُم مِّرۡفَقٗا

Na mlipotengana na watu wenu kwa ajili ya dini yenu na mkawaacha waungu wanaowaabudu isipokuwa kumuabudu Mungu Mmoja, basi hamieni kwenye pango iliyoko jabalini mpate kumuabudu Mola wenu Peke Yake, hapo Mwenyezi Mungu Atawakunjulia rehema Yake ambayo kwayo Atawapa sitara ya dunia na Akhera na Atawafanyia njia za maisha ziwe pesi mnufaike nazo katika maisha yenu. info
التفاسير:

external-link copy
17 : 18

۞ وَتَرَى ٱلشَّمۡسَ إِذَا طَلَعَت تَّزَٰوَرُ عَن كَهۡفِهِمۡ ذَاتَ ٱلۡيَمِينِ وَإِذَا غَرَبَت تَّقۡرِضُهُمۡ ذَاتَ ٱلشِّمَالِ وَهُمۡ فِي فَجۡوَةٖ مِّنۡهُۚ ذَٰلِكَ مِنۡ ءَايَٰتِ ٱللَّهِۗ مَن يَهۡدِ ٱللَّهُ فَهُوَ ٱلۡمُهۡتَدِۖ وَمَن يُضۡلِلۡ فَلَن تَجِدَ لَهُۥ وَلِيّٗا مُّرۡشِدٗا

Walipofanya hivyo, Mwenyezi Mungu Aliwatia usingizi wakalala na Akawahifadhi. Na utaliona jua, ewe mwenye kuwatazama wao, linapochomoza upande wa mashariki linapenyeza pale walipo upande wa kulia, na linapozama linawaacha upande wa kushoto, na hali wao wako kwenye sehemu kunjufu ndani ya pango, joto la jua haliwasumbui na hewa haiwakatikii. Hayo tuliyowafanyia vijana hawa ni miongoni mwa dalili za uweza wa wa Mwenyezi Mungu. Basi yoyote yule ambaye Mwenyezi Mungu Atamuafikia kuongoka kwa aya Zake, yeye ndiye mwenye kuongoka, na yoyote ambaye Hatamuafikia hilo, hutapata yoyote wa kumsaidia na kumuongoza kuifikia haki, kwani kuafikiwa na kutoafikiwa viko mikononi mwa Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
18 : 18

وَتَحۡسَبُهُمۡ أَيۡقَاظٗا وَهُمۡ رُقُودٞۚ وَنُقَلِّبُهُمۡ ذَاتَ ٱلۡيَمِينِ وَذَاتَ ٱلشِّمَالِۖ وَكَلۡبُهُم بَٰسِطٞ ذِرَاعَيۡهِ بِٱلۡوَصِيدِۚ لَوِ ٱطَّلَعۡتَ عَلَيۡهِمۡ لَوَلَّيۡتَ مِنۡهُمۡ فِرَارٗا وَلَمُلِئۡتَ مِنۡهُمۡ رُعۡبٗا

Na utadhani, ewe mwenye kutazama, kwamba watu wa pangoni wako katika hali ya kuangaza, na mambo yalivyo ni kuwa wao wamelala, na sisi tunawaangalia kwa kuwatunza, tunawageuza na wao wamelala, mara nyingine ubavu wa kulia na mara nyingine ubavu wa kushoto, ili ardhi isiwale, na mbwa wao aliyekuwa amefuatana nao ameinyosha miguu yake ya mbele kwenye ukumbi wa pango. Lau uliwashuhudia ungaligeuka kukimbia na unagalijawa na kicho kwa kuwaogopa. info
التفاسير:

external-link copy
19 : 18

وَكَذَٰلِكَ بَعَثۡنَٰهُمۡ لِيَتَسَآءَلُواْ بَيۡنَهُمۡۚ قَالَ قَآئِلٞ مِّنۡهُمۡ كَمۡ لَبِثۡتُمۡۖ قَالُواْ لَبِثۡنَا يَوۡمًا أَوۡ بَعۡضَ يَوۡمٖۚ قَالُواْ رَبُّكُمۡ أَعۡلَمُ بِمَا لَبِثۡتُمۡ فَٱبۡعَثُوٓاْ أَحَدَكُم بِوَرِقِكُمۡ هَٰذِهِۦٓ إِلَى ٱلۡمَدِينَةِ فَلۡيَنظُرۡ أَيُّهَآ أَزۡكَىٰ طَعَامٗا فَلۡيَأۡتِكُم بِرِزۡقٖ مِّنۡهُ وَلۡيَتَلَطَّفۡ وَلَا يُشۡعِرَنَّ بِكُمۡ أَحَدًا

Na kama tulivyowalaza na tukawahifadhi muda huu mrefu, tuliwaamsha kutoka kwenye usingizi wao kama vile walivyokuwa bila kubadilika, ili waulizane wao kwa wao, «Ni muda gani tulikaa tukiwa tumelala hapa?» Baadhi yao wakasema, «Tumekaa siku moja au sehemu ya siku.» Na wengine ambao mambo yaliwachanganyikia walisema, «utegemezeni ujuzi wa hilo kwa Mwenyezi Mungu, kwani Mola wenu ni Mjuzi zaidi wa kipindi mlichokikaa, basi mtumeni mmoja wenu na pesa zenu hizi za fedha aende mjini kwetu aangalie ni mtu gani hapo mjini mwenye chakula kizuri zaidi na cha halali, na awaletee chakula kutoka kwake, na ajifichefiche akiwa na muuzaji katika kununua kwake ili tusigundulike na mambo yetu yakafichuka, na msijulikane kabisa na mtu yoyote. info
التفاسير:

external-link copy
20 : 18

إِنَّهُمۡ إِن يَظۡهَرُواْ عَلَيۡكُمۡ يَرۡجُمُوكُمۡ أَوۡ يُعِيدُوكُمۡ فِي مِلَّتِهِمۡ وَلَن تُفۡلِحُوٓاْ إِذًا أَبَدٗا

Kwa hakika watu wenu wakiwagundua mulipo watawapiga mawe wawaue au watawarudisha kwenye dini yao muwe makafiri, na mkifanya hivyo basi hamtafaulu kabisa kupata matakwa yenu ya kuingia Peponi. info
التفاسير: