Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis

external-link copy
88 : 16

ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَصَدُّواْ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ زِدۡنَٰهُمۡ عَذَابٗا فَوۡقَ ٱلۡعَذَابِ بِمَا كَانُواْ يُفۡسِدُونَ

Wale ambao waliukanusha upweke wa Mwenyezi Mungu na unabii wako, ewe mtume, na wakakukanusha wewe, wakawakataza wengine wasimuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, tutawazidishia adhabu juu ya ukanushaji wao na adhabu juu ya kuwazuia watu kuifuata haki. Na hili ni kwa sababu ya kukusudia kwao kufanya uharibifu na kuwapoteza waja kwa ukafiri na uasi. info
التفاسير: