Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis

external-link copy
116 : 16

وَلَا تَقُولُواْ لِمَا تَصِفُ أَلۡسِنَتُكُمُ ٱلۡكَذِبَ هَٰذَا حَلَٰلٞ وَهَٰذَا حَرَامٞ لِّتَفۡتَرُواْ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَۚ إِنَّ ٱلَّذِينَ يَفۡتَرُونَ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَ لَا يُفۡلِحُونَ

wala msiseme, enyi washirikina, urongo unaotolewa na ndimi zenu: «hii ni halali» juu ya kitu kilichoharamishwa «na hii ni haramu» juu ya kitu kilichohalalishwa, ili kumzulia Mwenyezi Mungu urongo kwa kumnasibishia uhalalishaji na uharamishaji. Hakika wale wanaomzulia Mwenyezi Mungu urongo hawatafaulu kupata wema wowote ulimwenguni wala Akhera. info
التفاسير: