Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis

external-link copy
70 : 12

فَلَمَّا جَهَّزَهُم بِجَهَازِهِمۡ جَعَلَ ٱلسِّقَايَةَ فِي رَحۡلِ أَخِيهِ ثُمَّ أَذَّنَ مُؤَذِّنٌ أَيَّتُهَا ٱلۡعِيرُ إِنَّكُمۡ لَسَٰرِقُونَ

Na alipowatayarishia Yūsuf na akawabebesha chakula ngamia wao, aliwaamuru watumishi wake wakakiweka kile chombo, ambacho alikua akiwapimia nacho watu, kwenye vyombo vya ndugu yake Binyamin kwa namna ambayo asitambue yoyote. Basi walipopanda kwenda zao, aliita mwenye kuita akisema, «Enyi wenye ngamia waliobebeshwa chakula, nyinyi ni wezi!» info
التفاسير: