Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdullah Muhammad & Naser Khamis

external-link copy
8 : 11

وَلَئِنۡ أَخَّرۡنَا عَنۡهُمُ ٱلۡعَذَابَ إِلَىٰٓ أُمَّةٖ مَّعۡدُودَةٖ لَّيَقُولُنَّ مَا يَحۡبِسُهُۥٓۗ أَلَا يَوۡمَ يَأۡتِيهِمۡ لَيۡسَ مَصۡرُوفًا عَنۡهُمۡ وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُواْ بِهِۦ يَسۡتَهۡزِءُونَ

Na lau tutawacheleweshea adhabu, hawa washirikina, mpaka muda maalumu, wakaona imekawia, watasema kwa njia ya shere na kukanusha, «Ni kitu gani kinachozuia adhabu hii isitukie ikiwa ni kweli?» Jueni mtanabahi, siku itakapowajia adhabu hiyo hakuna atakayeweza kuwaondolea, wala yoyote mwenye kuizuia, na iatawazunguka wao, kutoka kila upande, adhabu waliokuwa wakiifanyia shere kabla haijawajia.. info
التفاسير: