[109] Hawi sawa katika itikadi yake wala katika vitendo vyake mwenye kusimamisha jengo lake kwa usafi wa niya katika kumcha Mwenyezi Mungu na kutafuta radhi zake, na yule mwenye kusimamisha jengo lake juu ya unaafiki, na ukafiri. Kwani vitendo vya mchamngu vimenyooka, vimejengeka juu ya msingi madhbuti. Na vitendo vya mnaafiki ni kama jengo lililo jengwa juu ya ukingo wa shimo. Jengo hilo litaporomoka tu, na litamtupa mwenyewe katika Moto wa Jahannamu. Na Mwenyezi Mungu hamuongoi kwenye Njia ya Uwongofu anaye shikilia kujidhulumu nafsi yake kwa ukafiri.