Übersetzung der Bedeutungen von dem heiligen Quran - Die Übersetzung in Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani.

Nummer der Seite:close

external-link copy
6 : 76

عَيۡنٗا يَشۡرَبُ بِهَا عِبَادُ ٱللَّهِ يُفَجِّرُونَهَا تَفۡجِيرٗا

Ni chemchem watakao inywa waja wa Mwenyezi Mungu, wakiifanya imiminike kwa wingi. info

Hiyo ni chemchem wanayo inywa waja wa Mwenyezi Mungu, na wanaipitisha watakapo kwa sahala.

التفاسير:

external-link copy
7 : 76

يُوفُونَ بِٱلنَّذۡرِ وَيَخَافُونَ يَوۡمٗا كَانَ شَرُّهُۥ مُسۡتَطِيرٗا

Wanatimiza ahadi,na wanaiogopa siku ambayo shari yake inaenea sana, info

Wanatekeleza yaliyo wajibikia , na wanaikhofu Siku kubwa hiyo ambayo madhara yake yataenea kote kote,

التفاسير:

external-link copy
8 : 76

وَيُطۡعِمُونَ ٱلطَّعَامَ عَلَىٰ حُبِّهِۦ مِسۡكِينٗا وَيَتِيمٗا وَأَسِيرًا

Na huwalisha chakula, juu ya kukipenda kwake, masikini, na yatima, na wafungwa. info

Na huwalisha chakula mafakiri wasio weza kazi, na watoto walio fiwa na wazee wao, na wafungwa wasio miliki kitu, ijapo kuwa wao wenyewe hao watoaji wanakipenda hicho wanacho kitoa, na wanakihitajia.

التفاسير:

external-link copy
9 : 76

إِنَّمَا نُطۡعِمُكُمۡ لِوَجۡهِ ٱللَّهِ لَا نُرِيدُ مِنكُمۡ جَزَآءٗ وَلَا شُكُورًا

Hakika sisi tunakulisheni kwa wajihi wa Mwenyezi Mungu. Hatutaki kwenu malipo wala shukrani. info

Na hujiambia nafsi zao: Hakika sisi tunakulisheni kwa ajili ya kutaka thawa;bu za Mwenyezi Mungu. Sisi hatutaki kwenu malipo au zawadi, wala hatutaki kushukuriwa na kusifiwa.

التفاسير:

external-link copy
10 : 76

إِنَّا نَخَافُ مِن رَّبِّنَا يَوۡمًا عَبُوسٗا قَمۡطَرِيرٗا

Hakika sisi tunaiogopa kwa Mola wetu Mlezi hiyo siku yenye shida na taabu. info

Hakika sisi tunakhofu kwa Mola wetu Mlezi hiyo siku ya kumletea msiba atakaye kuwapo siku hiyo, na siku ya watu kukunja nyuso zao na vipaji vyao.

التفاسير:

external-link copy
11 : 76

فَوَقَىٰهُمُ ٱللَّهُ شَرَّ ذَٰلِكَ ٱلۡيَوۡمِ وَلَقَّىٰهُمۡ نَضۡرَةٗ وَسُرُورٗا

Basi Mwenyezi Mungu atwalinda na shari ya siku hiyo, na atawakutanisha na raha na furaha. info

Basi Mwenyezi Mungu akawalinda na shida za siku hiyo, na badala ya mkunjo wa wenye maasi, akawapa nyuso za kupendeza, na ukunjufu na furaha katika nyoyo zao,

التفاسير:

external-link copy
12 : 76

وَجَزَىٰهُم بِمَا صَبَرُواْ جَنَّةٗ وَحَرِيرٗا

Na atawajazi Bustani za Peponi na maguo ya hariri kwa vile walivyo subiri. info

Na akawajazi kwa ile subira yao Pepo imeenea furaha, na nguo zake ni hariri laini.

التفاسير:

external-link copy
13 : 76

مُّتَّكِـِٔينَ فِيهَا عَلَى ٱلۡأَرَآئِكِۖ لَا يَرَوۡنَ فِيهَا شَمۡسٗا وَلَا زَمۡهَرِيرٗا

Humo wataegemea juu ya viti vya enzi, hawataona humo jua kali wala baridi kali. info

Wakiegemea huko Peponi juu ya makochi, hawaoni joto la jua, wala shida ya baridi.

التفاسير:

external-link copy
14 : 76

وَدَانِيَةً عَلَيۡهِمۡ ظِلَٰلُهَا وَذُلِّلَتۡ قُطُوفُهَا تَذۡلِيلٗا

Na vivuli vyake vitakuwa karibu yao, na mashada ya matunda yataning'inia mpaka chini. info

Na Pepo ambayo vivuli vya miti yake vimeenea kote kote, na matunda yake mepesi kuyachuma.

التفاسير:

external-link copy
15 : 76

وَيُطَافُ عَلَيۡهِم بِـَٔانِيَةٖ مِّن فِضَّةٖ وَأَكۡوَابٖ كَانَتۡ قَوَارِيرَا۠

Na watapitishiwa vyombo vya fedha na vikombe vya vigae, info

Na wakiwazungukia watumishi wao kwa bilauri za kunywea zilio fanywa kwa fedha, lakini unaona kiliomo ndani kama kwamba ni kigae,

التفاسير:

external-link copy
16 : 76

قَوَارِيرَاْ مِن فِضَّةٖ قَدَّرُوهَا تَقۡدِيرٗا

Vya fedha safi kama kiyoo, wamevipima kwa vipimo. info

Na vinapimwa vinywaji kwa kadiri wanavyo penda wanywaji.

التفاسير:

external-link copy
17 : 76

وَيُسۡقَوۡنَ فِيهَا كَأۡسٗا كَانَ مِزَاجُهَا زَنجَبِيلًا

Na humo watanyweshwa kinywaji kilicho changanyika na tangawizi. info

Na watu wema hupewa kunywa huko Peponi mvinyo inayo fanana na sharubati ya tangawizi kwa utamu.

التفاسير:

external-link copy
18 : 76

عَيۡنٗا فِيهَا تُسَمَّىٰ سَلۡسَبِيلٗا

Hiyo ni chemchem iliyo humo inaitwa Salsabil. info

Hiyo ni kutokana na chemchem ya Peponi inayo itwa Salsabil, kwa sababu ya wepesi wa unywaji wake na uzuri wake.

التفاسير:

external-link copy
19 : 76

۞ وَيَطُوفُ عَلَيۡهِمۡ وِلۡدَٰنٞ مُّخَلَّدُونَ إِذَا رَأَيۡتَهُمۡ حَسِبۡتَهُمۡ لُؤۡلُؤٗا مَّنثُورٗا

Na watawazungukia kuwatumikia wavulana wasio pevuka, ukiwaona utawafikiri ni lulu zilizo tawanywa. info

Na watakuwa wanawazunguka vijana ambao hawabadiliki hali yao, kwa furaha na sururi. Ukiwaona wanapo zunguka kwa wepesi na uchangamfu, utawadhania kwa uzuri wao na usafi wa rangi zao, kama lulu zilizo tandazwa mbele yako zinang'ara.

التفاسير:

external-link copy
20 : 76

وَإِذَا رَأَيۡتَ ثَمَّ رَأَيۡتَ نَعِيمٗا وَمُلۡكٗا كَبِيرًا

Na utakapo yaona, utakuwa umeona neema na ufalme mkubwa. info

Na ukitazama popote katika hiyo Pepo utaona neema kubwa, na ufalme ulio tanda.

التفاسير:

external-link copy
21 : 76

عَٰلِيَهُمۡ ثِيَابُ سُندُسٍ خُضۡرٞ وَإِسۡتَبۡرَقٞۖ وَحُلُّوٓاْ أَسَاوِرَ مِن فِضَّةٖ وَسَقَىٰهُمۡ رَبُّهُمۡ شَرَابٗا طَهُورًا

Juu yao zipo nguo za hariri laini za kijani kibichi, na hariri nzito ya at'ilasi. Na watavikwa vikuku vya fedha, na Mola wao Mlezi atawanywesha kinywaji safi kabisa. info

Juu yao zipo nguo za hariri nyepesi za kijani, na nguo za hariri nzito. Na mapambo yao yaliomo mikononi mwao ni vikuku vya fedha. Na Mola wao Mlezi atawanywesha kinywaji kingine kilio safi, hakina uchafu wala najisi.

التفاسير:

external-link copy
22 : 76

إِنَّ هَٰذَا كَانَ لَكُمۡ جَزَآءٗ وَكَانَ سَعۡيُكُم مَّشۡكُورًا

Hakika haya ni malipo yenu; na juhudi zenu zimekubaliwa. info

Hakika neema hizi ameziandaa kwa kukulipeni kwa vitendo vyenu. Na hizo juhudi zenu duniani ni zenye kusifika kwa Mwenyezi Mungu, na zinampendeza, na zimekubaliwa.

التفاسير:

external-link copy
23 : 76

إِنَّا نَحۡنُ نَزَّلۡنَا عَلَيۡكَ ٱلۡقُرۡءَانَ تَنزِيلٗا

Hakika Sisi tumekuteremshia Qur'ani kidogo kidogo. info

Hakika Sisi, kwa rehema yetu na hikima yetu, tumekuteremshia wewe Qur'ani kwa njia ya kukutuza moyo wako, na uweze daima kuihifadhi, basi huto isahau kabisa.

التفاسير:

external-link copy
24 : 76

فَٱصۡبِرۡ لِحُكۡمِ رَبِّكَ وَلَا تُطِعۡ مِنۡهُمۡ ءَاثِمًا أَوۡ كَفُورٗا

Basi ngojea hukumu ya Mola wako Mlezi wala usimt'ii miongoni mwao mwenye dhambi au mwenye kufuru. info

Basi subiri, uivumilie hikima ya Mola wako Mlezi kwa kuakhirisha kushinda kwako kuwashinda maadui zako, na wewe ukapata mitihani kwa maudhi yao. Wala usiwat'ii washirikina, wingi wa madhambi, walio zama katika ukafiri.

التفاسير:

external-link copy
25 : 76

وَٱذۡكُرِ ٱسۡمَ رَبِّكَ بُكۡرَةٗ وَأَصِيلٗا

Na likumbuke jina la Mola wako Mlezi asubuhi na jioni; info

Na dumisha kumkumbuka na kumtaja Mola wako Mlezi, na sali alfajiri mapema, na adhuhuri, na alasiri jioni,

التفاسير: