[54] Waambie: Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume kwa ut'iifu wa kweli wenye kuonyesha vitendo vyenu. Wanaafiki wakipuuza wasifuate, basi juu ya Muhammad ni waajibu wa aliyo twishwa tu na Mwenyezi Mungu, nayo ni amri ya kufikilisha Ujumbe, wala hakukalifishwa uwongofu wao. Na nyinyi juu yenu ni hayo aliyo kutwikeni Mwenyezi Mungu nayo ni kufuata na kut'ii. Na mtapata adhabu ikiwa mtaendelea na uasi. Na mkimt'ii Mtume mtaongoka kwenye kheri. Na yeye haimpasi ila kufikisha kwa uwazi mukimti au mukiamsi na yeye akaisha fikisha