Übersetzung der Bedeutungen von dem heiligen Quran - Die Übersetzung in Swahili

Nummer der Seite:close

external-link copy
26 : 76

وَمِنَ ٱلَّيۡلِ فَٱسۡجُدۡ لَهُۥ وَسَبِّحۡهُ لَيۡلٗا طَوِيلًا

Na wakati wa usiku, mnyenyekee Mola wako na umswalie na umuabudu kipindi kirefu cha usiku. info
التفاسير:

external-link copy
27 : 76

إِنَّ هَٰٓؤُلَآءِ يُحِبُّونَ ٱلۡعَاجِلَةَ وَيَذَرُونَ وَرَآءَهُمۡ يَوۡمٗا ثَقِيلٗا

Kwa hakika hawa washirikina wanaupenda ulimwengu na wanaushughulikia, na wanakuacha nyuma ya migongo yao kule kufanya matendo ya kuwafaa Akhera na kuwaokoa katika Siku yenye shida kubwa. info
التفاسير:

external-link copy
28 : 76

نَّحۡنُ خَلَقۡنَٰهُمۡ وَشَدَدۡنَآ أَسۡرَهُمۡۖ وَإِذَا شِئۡنَا بَدَّلۡنَآ أَمۡثَٰلَهُمۡ تَبۡدِيلًا

Sisi Ndio tuliowaumba na tukalipa uthabiti umbo lao. Na tunapotaka tunawaangamiza na kuwaleta watu walio watiifu zaidi wa Mwenyezi Mungu kuliko wao. info
التفاسير:

external-link copy
29 : 76

إِنَّ هَٰذِهِۦ تَذۡكِرَةٞۖ فَمَن شَآءَ ٱتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِۦ سَبِيلٗا

Hakika ndani ya sura hii, kwa yaliyomo ya kuvutia na kuogopesha, ya kuahidi mema na kuonya mabaya, kuna mawaidha kwa viumbe wote. Basi mwenye kujitakia wema nafsi yake ya duniani na Akhera, na ashike njia ya Imani na uchamungu itakayomfikisha kwenye msamaha wa Mwenyezi Mungu na radhi Zake. info
التفاسير:

external-link copy
30 : 76

وَمَا تَشَآءُونَ إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمٗا

Na hamtataka jambo lolote miongoni mwa mambo isipokuwa kwa makadirio ya Mwenyezi Mungu na matakwa Yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa hali za viumbe Vyake, ni Mwingi wa hekima katika uendeshaji na utengezaji Wake. info
التفاسير:

external-link copy
31 : 76

يُدۡخِلُ مَن يَشَآءُ فِي رَحۡمَتِهِۦۚ وَٱلظَّٰلِمِينَ أَعَدَّ لَهُمۡ عَذَابًا أَلِيمَۢا

Anamuingiza Anayemtaka miongoni mwa waja Wake katika rehema Yake na radhi Yake, na wao ni wale walioamini. Na Amewaandalia madhalimu waliokiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu adhabu yenye kuumiza. info
التفاسير: