Übersetzung der Bedeutungen von dem heiligen Quran - Die Übersetzung in Swahili

Al-Furqan

external-link copy
1 : 25

تَبَارَكَ ٱلَّذِي نَزَّلَ ٱلۡفُرۡقَانَ عَلَىٰ عَبۡدِهِۦ لِيَكُونَ لِلۡعَٰلَمِينَ نَذِيرًا

Ni kubwa mno baraka za Mwenyezi Mungu na ni mengi sana mema Yake na ni kamilifu sifa Zake, Aliyetakasika na kutukuka, Ambaye Ameiteremsha Qur’ani, yenye kupambanua baina ya ukweli na ubatilifu, kwa mja Wake Muhammad, rehemea ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ili awe ni mjumbe kwa binadamu na majini na awe muonyaji wa adhabu ya Mwenyezi Mungu kwao. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 25

ٱلَّذِي لَهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَلَمۡ يَتَّخِذۡ وَلَدٗا وَلَمۡ يَكُن لَّهُۥ شَرِيكٞ فِي ٱلۡمُلۡكِ وَخَلَقَ كُلَّ شَيۡءٖ فَقَدَّرَهُۥ تَقۡدِيرٗا

Ambaye Ana ufalme wa mbingu na ardhi, Hakujifanyia mtoto na hakuwa na mshirika katika ufalme Wake. Na Yeye Ndiye Aliyeumba kila kitu, Akakisawazisha kulingana na umbo linalonasibiana nacho na inavyotakikana kulingana na hekima Yake, pasi na kupungua wala kwenda kombo. info
التفاسير: