Übersetzung der Bedeutungen von dem heiligen Quran - Die Übersetzung in Swahili

Nummer der Seite:close

external-link copy
36 : 21

وَإِذَا رَءَاكَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ إِن يَتَّخِذُونَكَ إِلَّا هُزُوًا أَهَٰذَا ٱلَّذِي يَذۡكُرُ ءَالِهَتَكُمۡ وَهُم بِذِكۡرِ ٱلرَّحۡمَٰنِ هُمۡ كَٰفِرُونَ

Na makafiri wanapokuona, ewe Mtume, wanakuashiria kwa kukufanyia shere, huwa wakiambiana wao kwa wao, «Je, ni huyu yule mtu anayewatukana waungu wenu?» Wao wamemkanusha Mwingi wa rehema na wamezikanusha neema Zake na yale Aliyoyateremsha ya Qur’ani na uongofu. info
التفاسير:

external-link copy
37 : 21

خُلِقَ ٱلۡإِنسَٰنُ مِنۡ عَجَلٖۚ سَأُوْرِيكُمۡ ءَايَٰتِي فَلَا تَسۡتَعۡجِلُونِ

Ameumbwa mwanadamu akiwa na pupa, anayafanyia haraka mambo na anakuwa na pupa yawe. Na kwa kweli, Makureshi waliifanyia haraka adhabu na wakaona kuwa imechelewa kutokea., Mwenyezi Mungu Akawaonya kwamba Atawaonesha adhabu waliyoifanyia haraka, basi wasimuombe Mwenyezi Mungu awaharakishie na awaletee kwa upesi. info
التفاسير:

external-link copy
38 : 21

وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَٰذَا ٱلۡوَعۡدُ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Na makafiri wanasema, wakiifanyia haraka adhabu kwa njia ya shere, «Ni lini itapatikana ile unayotuonya nayo, ewe Muhammad, iwapo wewe na aliyekufuata wewe ni miongoni mwa wakweli.» info
التفاسير:

external-link copy
39 : 21

لَوۡ يَعۡلَمُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ حِينَ لَا يَكُفُّونَ عَن وُجُوهِهِمُ ٱلنَّارَ وَلَا عَن ظُهُورِهِمۡ وَلَا هُمۡ يُنصَرُونَ

Lau makafiri wanajua watakayoyakuta watakapokuwa hawawezi kuzilinda nyuso zao na migongo yao na Moto na wasiipate wenye kuwanusuru, hawangalibaki kwenye ukafiri wao na hawangaliifanyia haraka adhabu yao. info
التفاسير:

external-link copy
40 : 21

بَلۡ تَأۡتِيهِم بَغۡتَةٗ فَتَبۡهَتُهُمۡ فَلَا يَسۡتَطِيعُونَ رَدَّهَا وَلَا هُمۡ يُنظَرُونَ

Hakika Kiyama kitawajia ghafla, hapo wataduwaa na watakuwa na kicho kikubwa na hawataweza kuizuia adhabu isiwapate, na hawatapewa nafasi ya kutubia wala kutoa udhuru. info
التفاسير:

external-link copy
41 : 21

وَلَقَدِ ٱسۡتُهۡزِئَ بِرُسُلٖ مِّن قَبۡلِكَ فَحَاقَ بِٱلَّذِينَ سَخِرُواْ مِنۡهُم مَّا كَانُواْ بِهِۦ يَسۡتَهۡزِءُونَ

Mitume kabla yako, ewe Mtume, walifanyiwa shere, ikawafikia wale waliokuwa wakiifanyia shere adhabu ambayo walikiifanyia dhihaka na kejeli. info
التفاسير:

external-link copy
42 : 21

قُلۡ مَن يَكۡلَؤُكُم بِٱلَّيۡلِ وَٱلنَّهَارِ مِنَ ٱلرَّحۡمَٰنِۚ بَلۡ هُمۡ عَن ذِكۡرِ رَبِّهِم مُّعۡرِضُونَ

Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa wanaoifanyia haraka adhabu, «Hakuna anayewahifadhi na kuwalinda na adhabu ya Mwenyezi Mungu ikiwashukia , usiku wenu au mchana wenu, katika kulala kwenu au kuangaza kwenu?» Bali wao wamepumbaa na wameghafilika na Qur’ani na mawaidha. info
التفاسير:

external-link copy
43 : 21

أَمۡ لَهُمۡ ءَالِهَةٞ تَمۡنَعُهُم مِّن دُونِنَاۚ لَا يَسۡتَطِيعُونَ نَصۡرَ أَنفُسِهِمۡ وَلَا هُم مِّنَّا يُصۡحَبُونَ

Je wao wanao waungu wenye kuwazuia wao na adhabu yetu? Kwa hakika, waola wao hawawezi kujinusuru wenyewe, vipi wataweza kuwanusuru wenye kuwaabudu? Na wao hawatanusuriwa kutokana na sisi. info
التفاسير:

external-link copy
44 : 21

بَلۡ مَتَّعۡنَا هَٰٓؤُلَآءِ وَءَابَآءَهُمۡ حَتَّىٰ طَالَ عَلَيۡهِمُ ٱلۡعُمُرُۗ أَفَلَا يَرَوۡنَ أَنَّا نَأۡتِي ٱلۡأَرۡضَ نَنقُصُهَا مِنۡ أَطۡرَافِهَآۚ أَفَهُمُ ٱلۡغَٰلِبُونَ

Kwa hakika makafiri na baba zao walighurika na muhula waliopewa kwa kile walichokiona cha mali, watoto na maisha marefu, ndipo wakajikita kwenye ukafiri wao wasiepukane nao, na wakadhani kwamba wao hawataadhibiwa. Kwa kweli, wameghafilika na mpango uliopita, kwani Mwenyezi Mungu anaipunguza ardhi kwenye pambizo zake kwa adhabu Anayoiteremsha kwa washirikina kila sehemu na kushindwa. Je, makafiri wa Makkah Wana nafasi ya kutoka nje ya uwezo wa Mwenyezi Mungu au kukataa kufa? info
التفاسير: