Prijevod značenja časnog Kur'ana - Prijevod na svahili jezik: Alija Muhsin el-Bervani.

Az-Zalzalah

external-link copy
1 : 99

إِذَا زُلۡزِلَتِ ٱلۡأَرۡضُ زِلۡزَالَهَا

Itakapo tetemeshwa ardhi kwa mtetemeko wake! info

Ikitisika ardhi kwa mtikiso mkubwa, na ikasukika kwa ukomo wa kutisika na kusukika kunako mkinika na ikaweza kuchukua!

التفاسير:

external-link copy
2 : 99

وَأَخۡرَجَتِ ٱلۡأَرۡضُ أَثۡقَالَهَا

Na itakapo toa ardhi mizigo yake! info

Na ardhi ikatoa yote yaliomo katika ndani ya tumbo lake, ikiwa khazina au maiti walio kwisha zikwa!

التفاسير:

external-link copy
3 : 99

وَقَالَ ٱلۡإِنسَٰنُ مَا لَهَا

Na mtu akasema: Ina nini? info

Na binaadamu akasema kwa kushtuka na khofu: Ardhi hii ina nini hata inatikisika hivi, na inatoa vilivyomo tumboni mwake, ndio Saa imefika?

التفاسير:

external-link copy
4 : 99

يَوۡمَئِذٖ تُحَدِّثُ أَخۡبَارَهَا

Siku hiyo itahadithia khabari zake. info

Siku hiyo ardhi itamsimulia mtu khabari zake zilio mshitua,

التفاسير:

external-link copy
5 : 99

بِأَنَّ رَبَّكَ أَوۡحَىٰ لَهَا

Kwa sababu Mola wake Mlezi ameifunulia! info

Kwani Mlezi wake na Muumba wake atakuwa kaifunulia, kaipa Wahyi, na kaiamuru itetemeke na ijisuke suke, ndio ikafanya upesi kutekeleza amri.

التفاسير:

external-link copy
6 : 99

يَوۡمَئِذٖ يَصۡدُرُ ٱلنَّاسُ أَشۡتَاتٗا لِّيُرَوۡاْ أَعۡمَٰلَهُمۡ

Siku hiyo watu watatoka kwa mfarakano wakaonyweshwe vitendo vyao! info

Siku hiyo watu watatoka makaburini mbio, nao wamo katika mtafaruku, wapate kuziona hisabu zao na malipo yao aliyo waahidi Mwenyezi Mungu.

التفاسير:

external-link copy
7 : 99

فَمَن يَعۡمَلۡ مِثۡقَالَ ذَرَّةٍ خَيۡرٗا يَرَهُۥ

Basi anaye tenda chembe ya wema, atauona! info

Basi mwenye kufanya hata kitu chenye uzito wa punje ya mchanga cha kheri ataiona katika daftari lake, na atapata malipo yake.

التفاسير:

external-link copy
8 : 99

وَمَن يَعۡمَلۡ مِثۡقَالَ ذَرَّةٖ شَرّٗا يَرَهُۥ

Na anaye tenda chembe ya uovu atauona! info

Na mwenye kufanya shari ya uzito wa chembe ya mchanga ataiona kadhaalika, na atapata malipo yake. Wala Mola wako Mlezi hatamdhulumu yeyote.

التفاسير: