Prijevod značenja časnog Kur'ana - Prijevod na svahili jezik: Alija Muhsin el-Bervani.

Broj stranice:close

external-link copy
91 : 15

ٱلَّذِينَ جَعَلُواْ ٱلۡقُرۡءَانَ عِضِينَ

Ambao wakaifanya Qur'ani vipande vipande. info

Hao waliifanya Qur'ani vipande mbali mbali, nayo hali kuwa haikubali kugawika kwa umuujiza wake na ukweli wake.

التفاسير:

external-link copy
92 : 15

فَوَرَبِّكَ لَنَسۡـَٔلَنَّهُمۡ أَجۡمَعِينَ

Basi Naapa kwa Mola wako Mlezi! Tutawahoji wote. info

Ikiwa hiyo hali yao, basi Wallahi kwa Aliye kuumba akakulinda na akakulea, hapana shaka tutawahisabu wote Siku ya Kiyama,

التفاسير:

external-link copy
93 : 15

عَمَّا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Kwa waliyo kuwa wakiyatenda. info

Kwa vitendo vyao vya kuudhi, na kufuru, na kejeli.

التفاسير:

external-link copy
94 : 15

فَٱصۡدَعۡ بِمَا تُؤۡمَرُ وَأَعۡرِضۡ عَنِ ٱلۡمُشۡرِكِينَ

Basi wewe yatangaze uliyo amrishwa, na jitenge na washirikina. info

Basi wewe tangaza wito wa Haki, wala usishughulike na wayatendao washirikina na maneno yao.

التفاسير:

external-link copy
95 : 15

إِنَّا كَفَيۡنَٰكَ ٱلۡمُسۡتَهۡزِءِينَ

Hakika Sisi tunatosha kukukinga na wanao kejeli. info

Na hao washirikina wanao ukejeli wito wako hawatokushinda, wala hawatoweza kukuingilia kati baina yako na wito wako.

التفاسير:

external-link copy
96 : 15

ٱلَّذِينَ يَجۡعَلُونَ مَعَ ٱللَّهِ إِلَٰهًا ءَاخَرَۚ فَسَوۡفَ يَعۡلَمُونَ

Hao wanao fanya kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu yupo mungu mwingine.Basi, watakuja jua! info

Hao washirikina mawazo yao yamedhoofika, ndio wakafanya kuwa Mwenyezi Mungu anao miungu mingine ya masanamu. Na watakuja jua matokeo ya ushirikina wao itapo wateremkia adhabu chungu.

التفاسير:

external-link copy
97 : 15

وَلَقَدۡ نَعۡلَمُ أَنَّكَ يَضِيقُ صَدۡرُكَ بِمَا يَقُولُونَ

Na Sisi tunajua kwa hakika kuwa wewe kifua chako kinaona dhiki kwa hayo wayasemayo. info

Nasi tunajua dhiki ya moyo inayo kupata kwa wanayo yasema ya ushirikina na kejeli na dharau.

التفاسير:

external-link copy
98 : 15

فَسَبِّحۡ بِحَمۡدِ رَبِّكَ وَكُن مِّنَ ٱلسَّٰجِدِينَ

Basi mtakase Mola wako Mlezi kwa kumhimidi, na uwe miongoni wanaomsujudia. info

Ikikupata dhiki hiyo mkimbilie Mwenyezi Mungu Mtukufu umwelekee, na umt'ii na umnyenyekee, na utake msaada kwa Sala, kwani humo ndio imo poza.

التفاسير:

external-link copy
99 : 15

وَٱعۡبُدۡ رَبَّكَ حَتَّىٰ يَأۡتِيَكَ ٱلۡيَقِينُ

Na muabudu Mola wako Mlezi mpaka ikufikie Yakini. (nao ni Mauti) info

Na shikilia ibada ya Mwenyezi Mungu aliye kuumba, akakulinda, mpaka ifike amri ya yakini, nayo ni Mauti.

التفاسير: