Prijevod značenja časnog Kur'ana - Prijevod na svahili jezik - Abdullah Muhammed i Nasir Hamis

Al-A'la

external-link copy
1 : 87

سَبِّحِ ٱسۡمَ رَبِّكَ ٱلۡأَعۡلَى

Takasa Jina la Mola wako Aliyetukuka na kuepukana na mshirika na kila sifa pungufu kwa namna inayonasibiana na utukufu Wake na utakatifu Wake. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 87

ٱلَّذِي خَلَقَ فَسَوَّىٰ

Aliyeumba viumbe Akalitengeneza umbo lao na kulifanya zuri. info
التفاسير:

external-link copy
3 : 87

وَٱلَّذِي قَدَّرَ فَهَدَىٰ

Na Aliyekadiria kila kitu na kukipeleka njia inayonasibiana nacho. info
التفاسير:

external-link copy
4 : 87

وَٱلَّذِيٓ أَخۡرَجَ ٱلۡمَرۡعَىٰ

Na Aliyeotesha nyasi mbiti zenye rangi ya kijani, info
التفاسير:

external-link copy
5 : 87

فَجَعَلَهُۥ غُثَآءً أَحۡوَىٰ

Akazifanya baadaye kuwa kavu zilizobadilika rangi. info
التفاسير:

external-link copy
6 : 87

سَنُقۡرِئُكَ فَلَا تَنسَىٰٓ

Tutakusomea, ewe Mtume, hii Qur’ani kisomo ambacho hutakisahau. info
التفاسير:

external-link copy
7 : 87

إِلَّا مَا شَآءَ ٱللَّهُۚ إِنَّهُۥ يَعۡلَمُ ٱلۡجَهۡرَ وَمَا يَخۡفَىٰ

Isipokuwa iwapo Mwenyezi Mungu Ataka usahau kwa hekima na maslahi anayoyajua Yeye. Kwani Yeye ni Mjuzi wa yaliyo wazi na yaliyofichika, ya maneno na ya vitendo. info
التفاسير:

external-link copy
8 : 87

وَنُيَسِّرُكَ لِلۡيُسۡرَىٰ

Tutakufanyia mapesi mambo yako yote; miongoni mwayo ni kukusahilishia kubeba majukumu ya utume na kuifanya nyepesi Dini uliyokuja nayo. info
التفاسير:

external-link copy
9 : 87

فَذَكِّرۡ إِن نَّفَعَتِ ٱلذِّكۡرَىٰ

Basi wawaidhie kaumu zako, ewe Mtume, kwa namna tulivyokutayarishia ufanye kwenye wahyi ulioletewa, uwaongoze njia yenye kheri na wao na uwahusu kwa mawaidha yako wale wanaotarajiwa kuwaidhika nayo. Wala usijisumbue kuwashauri wale ambao mawidha hayawaathiri isipokuwa kuwatia ujeuri na kuwafanya wayakimbie. info
التفاسير:

external-link copy
10 : 87

سَيَذَّكَّرُ مَن يَخۡشَىٰ

Atanufaika kwa mawaidha anayemcha Mola wke, info
التفاسير:

external-link copy
11 : 87

وَيَتَجَنَّبُهَا ٱلۡأَشۡقَى

na atajiepusha na mawaidha aliye mbaya asiyemuogopa Mola wake info
التفاسير:

external-link copy
12 : 87

ٱلَّذِي يَصۡلَى ٱلنَّارَ ٱلۡكُبۡرَىٰ

atakayeingia kwenye Moto wa Jahanamu akiadhibika kwa ukali wake. info
التفاسير:

external-link copy
13 : 87

ثُمَّ لَا يَمُوتُ فِيهَا وَلَا يَحۡيَىٰ

Kisha hatakuwa ni mwenye kufa akapumzika wala ni mwenye kuishi akanufaika. info
التفاسير:

external-link copy
14 : 87

قَدۡ أَفۡلَحَ مَن تَزَكَّىٰ

Hakika amefuzu mwenye kuisafisha nafsi yake na tabia mbovu, info
التفاسير:

external-link copy
15 : 87

وَذَكَرَ ٱسۡمَ رَبِّهِۦ فَصَلَّىٰ

na akamtaja Mwenyezi Mungu, akampwekesha, akamuomba, akafanya vitendo vya kumridhisha na akasimamisha Swala kwa nyakati zake kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu na kufuata sheria Aliyoiweka. info
التفاسير:

external-link copy
16 : 87

بَلۡ تُؤۡثِرُونَ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا

Hakika yenu, nyinyi watu, mnafadhilisha pambo la maisha ya kilimwengu juu ya starehe za Akhera. info
التفاسير:

external-link copy
17 : 87

وَٱلۡأٓخِرَةُ خَيۡرٞ وَأَبۡقَىٰٓ

Na hakika ya mambo ni kuwa nyumba ya Akhera na starehe zake ni bora zaidi kuliko ulimwngu na ni yenye kusalia zaidi. info
التفاسير:

external-link copy
18 : 87

إِنَّ هَٰذَا لَفِي ٱلصُّحُفِ ٱلۡأُولَىٰ

Haya mlioosimuliwa ndani ya Sura hii ni miongoni mwa yaliyotajwa kimaana katika Kurasa zilizotangulia kuteremshwa kabla ya Qur’ani. info
التفاسير:

external-link copy
19 : 87

صُحُفِ إِبۡرَٰهِيمَ وَمُوسَىٰ

Nazo ni Kurasa za Ibrāhīm na Mūsā, amani ziwashukie. info
التفاسير: