Prijevod značenja časnog Kur'ana - Prijevod na svahili jezik - Abdullah Muhammed i Nasir Hamis

Broj stranice:close

external-link copy
17 : 56

يَطُوفُ عَلَيۡهِمۡ وِلۡدَٰنٞ مُّخَلَّدُونَ

Wanawazunguka wao kuwatumikia watumishi vijana wasiozeeka wala kufa, info
التفاسير:

external-link copy
18 : 56

بِأَكۡوَابٖ وَأَبَارِيقَ وَكَأۡسٖ مِّن مَّعِينٖ

wakiwa na vikombe, mabirika na gilasi kutoka kwenye chemchemi ya pombe yenye kupita ndani ya Pepo, info
التفاسير:

external-link copy
19 : 56

لَّا يُصَدَّعُونَ عَنۡهَا وَلَا يُنزِفُونَ

na hawaumwi na vichwa kutokana nayo wala hawarukwi na akili. info
التفاسير:

external-link copy
20 : 56

وَفَٰكِهَةٖ مِّمَّا يَتَخَيَّرُونَ

Na watawazunguka wao watumishi vijana na kila kitu wanachokichagua miongoni mwa matunda, info
التفاسير:

external-link copy
21 : 56

وَلَحۡمِ طَيۡرٖ مِّمَّا يَشۡتَهُونَ

nyama ya ndege ambayo nafsi zao inavutika nayo. info
التفاسير:

external-link copy
22 : 56

وَحُورٌ عِينٞ

Na watakuwa na wanawake wenye macho makubwa kama kwamba wao, info
التفاسير:

external-link copy
23 : 56

كَأَمۡثَٰلِ ٱللُّؤۡلُوِٕ ٱلۡمَكۡنُونِ

kwa usafi wao na uzuri wao, ni lulu iliyohifadhiwa ndani ya mashaza yake, info
التفاسير:

external-link copy
24 : 56

جَزَآءَۢ بِمَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

hali hayo yakiwa ni malipo yao kwa yale waliokuwa wakiyafanya duniani. info
التفاسير:

external-link copy
25 : 56

لَا يَسۡمَعُونَ فِيهَا لَغۡوٗا وَلَا تَأۡثِيمًا

Hawatasikia humo Peponi ubatilifu wala yale ya kuwatia madhambini kuyasikia, info
التفاسير:

external-link copy
26 : 56

إِلَّا قِيلٗا سَلَٰمٗا سَلَٰمٗا

isipokuwa maneno yasiyokuwa na kasoro hizi na kusalimiana wao kwa wao. info
التفاسير:

external-link copy
27 : 56

وَأَصۡحَٰبُ ٱلۡيَمِينِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلۡيَمِينِ

Na watu wa upande wa kulia, info
التفاسير:

external-link copy
28 : 56

فِي سِدۡرٖ مَّخۡضُودٖ

ni kikubwa kilioje cheo chao na malipo yao! info
التفاسير:

external-link copy
29 : 56

وَطَلۡحٖ مَّنضُودٖ

Watakuwa kwenye mikunazi isiyo na miba, na ndizi zilizopandana na kupangika, info
التفاسير:

external-link copy
30 : 56

وَظِلّٖ مَّمۡدُودٖ

kila ndizi juu ya nyingine, na vivuli vya daima visivyoondoka, info
التفاسير:

external-link copy
31 : 56

وَمَآءٖ مَّسۡكُوبٖ

na maji yanayotembea yasiyokatika, info
التفاسير:

external-link copy
32 : 56

وَفَٰكِهَةٖ كَثِيرَةٖ

na matunda mengi info
التفاسير:

external-link copy
33 : 56

لَّا مَقۡطُوعَةٖ وَلَا مَمۡنُوعَةٖ

yasiyomalizika wala kuwaishia wala hakuna kizuizi chochote kinachowazuia wao kuyafikia, info
التفاسير:

external-link copy
34 : 56

وَفُرُشٖ مَّرۡفُوعَةٍ

na matandiko yaliyoinuliwa juu ya vitanda. info
التفاسير:

external-link copy
35 : 56

إِنَّآ أَنشَأۡنَٰهُنَّ إِنشَآءٗ

Sisi tumewaumba wanawake wa watu wa Peponi umbile ambalo silo lile umbile lililokuwa duniani, umbile lililokamilika lisilokubali kutoweka, info
التفاسير:

external-link copy
36 : 56

فَجَعَلۡنَٰهُنَّ أَبۡكَارًا

na tumewafanya ni wanawali wenye kujipendekeza kwa waume zao, info
التفاسير:

external-link copy
37 : 56

عُرُبًا أَتۡرَابٗا

hali ya kuwa ni marika na wao kimiaka. info
التفاسير:

external-link copy
38 : 56

لِّأَصۡحَٰبِ ٱلۡيَمِينِ

Tumewaumbia wanawake hao watu wa upande wa kulia. info
التفاسير:

external-link copy
39 : 56

ثُلَّةٞ مِّنَ ٱلۡأَوَّلِينَ

Nao ni kundi la watu wengi wa mwanzo info
التفاسير:

external-link copy
40 : 56

وَثُلَّةٞ مِّنَ ٱلۡأٓخِرِينَ

na kundi la watu wengi wa mwisho. info
التفاسير:

external-link copy
41 : 56

وَأَصۡحَٰبُ ٱلشِّمَالِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلشِّمَالِ

Na watu wa upande wa kushoto, ni mbaya iliyoje hali yao na malipo yao! info
التفاسير:

external-link copy
42 : 56

فِي سَمُومٖ وَحَمِيمٖ

Watakuwa kwenye upepo ulio moto utokanao na joto la Moto wa Jahanamu utakaozuia pumzi zao, na maji moto yanayochemka, info
التفاسير:

external-link copy
43 : 56

وَظِلّٖ مِّن يَحۡمُومٖ

na kivuli cha moshi mweusi sana, info
التفاسير:

external-link copy
44 : 56

لَّا بَارِدٖ وَلَا كَرِيمٍ

usio na mashukio baridi wala mandhari mazuri. info
التفاسير:

external-link copy
45 : 56

إِنَّهُمۡ كَانُواْ قَبۡلَ ذَٰلِكَ مُتۡرَفِينَ

Kwani wao walikuwa duniani wakijistarehesha kwa vitu vya haramu wakijiepusha na yale ambayo Mitume walikuja nayo. info
التفاسير:

external-link copy
46 : 56

وَكَانُواْ يُصِرُّونَ عَلَى ٱلۡحِنثِ ٱلۡعَظِيمِ

Na walikuwa wamesimama wima katika kumkanusha Mwenyezi Mungu na kumshirikisha na kumuasi, na hawakuwa na nia ya kutubia kwa hayo. info
التفاسير:

external-link copy
47 : 56

وَكَانُواْ يَقُولُونَ أَئِذَا مِتۡنَا وَكُنَّا تُرَابٗا وَعِظَٰمًا أَءِنَّا لَمَبۡعُوثُونَ

Na walikuwa wakisema hali ya kukanusha Ufufuzi, «Je hivi sisi tutafufuliwa tutakapokufa na tukawa mchanga na mifupa iliyochakaa?» Maneno yao hayo yanaonesha kuwa wao walikuwa wakiliona jambo hili la kufufuliwa kuwa liko mbali na ukweli na wakilikanusha. info
التفاسير:

external-link copy
48 : 56

أَوَءَابَآؤُنَا ٱلۡأَوَّلُونَ

«Je tutafufuliwa sisi na hali baba zetu waliotangulia wamekuwa mchanga uliotapakaa kwenye ardhi?» info
التفاسير:

external-link copy
49 : 56

قُلۡ إِنَّ ٱلۡأَوَّلِينَ وَٱلۡأٓخِرِينَ

Sema uwaambie, «Hakika wa mwanzo na wa mwisho miongoni mwa binadamu info
التفاسير:

external-link copy
50 : 56

لَمَجۡمُوعُونَ إِلَىٰ مِيقَٰتِ يَوۡمٖ مَّعۡلُومٖ

watakusanywa katika Siku iliyowekewa wakati maalumu, nayo ni Siku ya Kiyama. info
التفاسير: