আল-কোৰআনুল কাৰীমৰ অৰ্থানুবাদ - শ্বাহিলি অনুবাদ- ৰুওৱাদ অনুবাদ চেণ্টাৰ

external-link copy
19 : 2

أَوۡ كَصَيِّبٖ مِّنَ ٱلسَّمَآءِ فِيهِ ظُلُمَٰتٞ وَرَعۡدٞ وَبَرۡقٞ يَجۡعَلُونَ أَصَٰبِعَهُمۡ فِيٓ ءَاذَانِهِم مِّنَ ٱلصَّوَٰعِقِ حَذَرَ ٱلۡمَوۡتِۚ وَٱللَّهُ مُحِيطُۢ بِٱلۡكَٰفِرِينَ

Au ni kama mvua kubwa itokayo mbinguni, ina viza mbalimbali, na radi, na umeme; wakawa wanatia vidole vyao katika masikio yao kwa sababu ya mapigo ya radi, kwa kuogopa kufa. Na Mwenyezi Mungu amewazunguka makafiri.[1] info

[1] Hapa Mwenyezi Mugnu aliufananisha uwongofu aliowaongoza kwao waja wake, na mvua. Kwa sababu, nyoyo huhuishwa kwa uwongofu, kama vile ardhi huhuishwa na mvua. Na fungu la wanafiki katika uwongofu huo ni kama fungu la yule ambaye hakupata katika mvua isipokuwa giza, radi na umeme, wala hana fungu zaidi ya hayo katika yale yaliyokusudiwa kutoka kwa mvua hiyo kama vile uhai wa nchi, watu, miti na wanyama. (Tafsir Ibn Al-Qayyim)

التفاسير: