ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني

سورة الطارق - At-Tariq

external-link copy
1 : 86

وَٱلسَّمَآءِ وَٱلطَّارِقِ

Naapa kwa mbingu na Kinacho kuja usiku! info

Naapa kwa mbingu na nyota inayo tokeza usiku!

التفاسير:

external-link copy
2 : 86

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلطَّارِقُ

Na nini kitakacho kujuulisha ni nini hicho Kinacho kuja usiku? info

Na kitu gani kitakujuvya ukweli wa nyota hii? Ni hiyo inayotoa mwanga wake katika giza.

التفاسير:

external-link copy
3 : 86

ٱلنَّجۡمُ ٱلثَّاقِبُ

Ni Nyota yenye mwanga mkali. info

Na kitu gani kitakujuvya ukweli wa nyota hii? Ni hiyo inayotoa mwanga wake katika giza.

التفاسير:

external-link copy
4 : 86

إِن كُلُّ نَفۡسٖ لَّمَّا عَلَيۡهَا حَافِظٞ

Hapana nafsi ila inayo mwangalizi. info

Hapana nafsi ila inayo mlinzi wa kuiangalia na kudhibiti vitendo vyake.

التفاسير:

external-link copy
5 : 86

فَلۡيَنظُرِ ٱلۡإِنسَٰنُ مِمَّ خُلِقَ

Hebu naajitazame mwanaadamu ameumbwa kwa kitu gani? info

Basi naafikiri mtu, yeye kaumbwa kutokana na nini?

التفاسير:

external-link copy
6 : 86

خُلِقَ مِن مَّآءٖ دَافِقٖ

Ameumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa! info

Ameumbwa mtu kutokana na maji yanayo toka kwa nguvu.

التفاسير:

external-link copy
7 : 86

يَخۡرُجُ مِنۢ بَيۡنِ ٱلصُّلۡبِ وَٱلتَّرَآئِبِ

Yatokayo baina ya mifupa ya mgongo na mbavu. info

Maji haya yanatoka baina ya uti wa mgongo na mbavu za mwanamume na mwanamke. S'ULB ni sehemu za uti wa mgongo; na TARAAIB ni mafupa ya vifua, yaani mbavu. Masomo ya watoto wanapo kuwa ndani ya matumbo ya mama zao (Embryology). yamedhihirisha kuwa viini vya vyombo vya uzazi na mkojo katika mtoto ndani ya tumbo la mama yake vinadhihiri baina ya khalaya (cells) za mishipa itakayo kuwa mafupa ya uti wa mgongo, na baina ya khalaya zitakazo kuwa mafupa ya kifua. Mafigo hubakia pahala pake, na kokwa huteremka kwenye pahala pake pa kawaida katika pumbu wakati wa kuzaliwa. Na juu ya kuteremka kokwa chini mishipa inayo inywesha damu maisha yake yote inatokana na mishipa ya mafigo. Hali kadhaalika mishipa ya Navo inayo peleka kuhisi na ikasaidia kuzalisha vitu vya uhai na yaliyo khusiana na hayo kama maji yanayo toka kwenye mshipa wa kifua wa kumi unao tokana na ubongo wa uti wa mgongo kwenye kipingili cha kumi na kumi na moja. Yaliyo wazi kutokana na hayo ni kwamba vyombo vya uzazi na vinavyo lisha vyombo hivyo, na vyombo vya damu, vipo katika kiwiliwili baina ya uti wa mgongo na mbavu.

التفاسير:

external-link copy
8 : 86

إِنَّهُۥ عَلَىٰ رَجۡعِهِۦ لَقَادِرٞ

Hakika Yeye ana uweza wa kumrudisha. info

Hakika Mwenyezi Mungu aliye muumba hivi hapo mwanzo, bila ya shaka ni Muweza wa kumuumba tena baada ya kufa kwake.

التفاسير:

external-link copy
9 : 86

يَوۡمَ تُبۡلَى ٱلسَّرَآئِرُ

Siku zitakapo dhihirishwa siri. info

Siku dhamiri zitapo fanyiwa mtihani, na zitengwe mbali mbali baina ya ziliyo kuwa nzuri na ziliyo kuwa mbovu.

التفاسير:

external-link copy
10 : 86

فَمَا لَهُۥ مِن قُوَّةٖ وَلَا نَاصِرٖ

Basi hatakuwa na nguvu wala msaidizi. info

Basi hapana mtu wakati huo ataye kuwa na nguvu ya kujikinga nafsi yake, wala hatakuwa na msaidizi wa kumnusuru.

التفاسير:

external-link copy
11 : 86

وَٱلسَّمَآءِ ذَاتِ ٱلرَّجۡعِ

Naapa kwa mbingu yenye marejeo! info

Naapa kwa mbingu yenye mvua inayo rejea na kuja mara kwa mara!

التفاسير:

external-link copy
12 : 86

وَٱلۡأَرۡضِ ذَاتِ ٱلصَّدۡعِ

Na kwa ardhi inayo pasuka! info

Na ardhi inayo pasuka kwa kuchipuka mimea!

التفاسير:

external-link copy
13 : 86

إِنَّهُۥ لَقَوۡلٞ فَصۡلٞ

Hakika hii ni kauli ya kupambanua. info

Hakika hii Qur'ani ni yenye kupambanua baina ya kweli na uwongo.

التفاسير:

external-link copy
14 : 86

وَمَا هُوَ بِٱلۡهَزۡلِ

Wala si mzaha. info

Wala haina nuksani yoyote ya mchezo au maskhara.

التفاسير:

external-link copy
15 : 86

إِنَّهُمۡ يَكِيدُونَ كَيۡدٗا

Hakika wao wanapanga mpango. info

Hakika hao wanao ikadhibisha Qur'ani wanaipangia njama kutaka kuiharibia, njama zenye kufikia ukomo!

التفاسير:

external-link copy
16 : 86

وَأَكِيدُ كَيۡدٗا

Na Mimi napanga mpango. info

Lakini Mimi nitawalipa, na nitavipambanisha hivyo vitimbi vyao kwa vitimbi madhubuti ambavyo hawataweza kujikinga navyo.

التفاسير:

external-link copy
17 : 86

فَمَهِّلِ ٱلۡكَٰفِرِينَ أَمۡهِلۡهُمۡ رُوَيۡدَۢا

Basi wape muhula makafiri - wape muhula pole pole. info

Basi wangojee hao makafiri! Wape muhula wa karibu mpaka nikuamrishe amri gani kali ya kuwatendea.

التفاسير: