Mfano wa Mayahudi walio funzwa Taurati, na wakalazimishwa waifuate, na wao hawakuifuata kwa vitendo, ni mfano wa punda aliye beba vitabu ambavyo hajui ndani yake mna nini. Ni mbaya mno mfano wa watu wanao kadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu hawasaidii kufikilia uwongofu watu ambao kazi yao ni kudhulumu.