ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني

سورة الجاثية - Al-Jathiyah

external-link copy
1 : 45

حمٓ

H'a Mim . info

H'a Mim. Hizi ni harufi mbili katika harufi za kutamkwa, zimeanzia Sura hii kama ada ya Sura nyingi katika Qur'ani ambazo zimeanzia kwa harufi kama hivi ili kuashiria kuwa washirikina wameshindwa kuleta mfano wake, ijapo kuwa hii Qur'ani imeundwa kwa harufi hizi hizi wanazo zitumia katika maneno yao.

التفاسير:

external-link copy
2 : 45

تَنزِيلُ ٱلۡكِتَٰبِ مِنَ ٱللَّهِ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡحَكِيمِ

Uteremsho wa Kitabu umetoka kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hikima. info

Huu mteremsho wa Qur'ani umetokana na Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Asiye shindika, Mwenye hikima katika kupanga kwake na kuendesha kwake.

التفاسير:

external-link copy
3 : 45

إِنَّ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ لَأٓيَٰتٖ لِّلۡمُؤۡمِنِينَ

Hakika katika mbingu na ardhi ziko Ishara kwa Waumini. info

Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi ni katika ufundi wa namna ya pekee wa Mwenyezi Mungu, bila ya shaka ni dalili zenye nguvu kabisa katika Ungu wake na Upweke wake, ambao wanauamini wenye kumsadiki Mwenyezi Mungu kwa maumbile yao yaliyo sawa.

التفاسير:

external-link copy
4 : 45

وَفِي خَلۡقِكُمۡ وَمَا يَبُثُّ مِن دَآبَّةٍ ءَايَٰتٞ لِّقَوۡمٖ يُوقِنُونَ

Na katika umbo lenu na katika wanyama alio watawanya zimo Ishara kwa watu wenye yakini. info

Na vile Mwenyezi Mungu kukuumbeni nyinyi, enyi watu, kama mlivyo, mna sura nzuri, na umbo la peke yenu, na mnavyo khitalifiana baina ya wanaadamu na wanyama na mkaenezwa ulimwenguni, na manufaa mbali mbali, bila ya shaka ni Ishara zenye nguvu na ziwazi kwa watu wanao tafuta yakini ya mambo yao kwa kuzingatia na kufikiri.

التفاسير:

external-link copy
5 : 45

وَٱخۡتِلَٰفِ ٱلَّيۡلِ وَٱلنَّهَارِ وَمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مِن رِّزۡقٖ فَأَحۡيَا بِهِ ٱلۡأَرۡضَ بَعۡدَ مَوۡتِهَا وَتَصۡرِيفِ ٱلرِّيَٰحِ ءَايَٰتٞ لِّقَوۡمٖ يَعۡقِلُونَ

Na kupishana usiku na mchana, na riziki anayo iteremsha Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni, na kwayo akaifufua ardhi baada ya kufa kwake, na mabadiliko ya upepo, ni Ishara kwa watu wenye akili. info

Na katika kukhitalifiana usiku na mchana, kwa urefu na ufupi, na mwangaza na giza, na kupeana zamu kwa nidhamu iliyo thibiti, na katika mvua anayo iteremsha Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni, akaihuisha ardhi kwa mimea baada ya kufa kwake kwa ukame, na kuziendesha pepo pande mbali mbali nazo zinakhitalifiana kwa ubaridi na joto, na nguvu na udhaifu, ni alama zilizo wazi za kuonyesha ukamilifu wa uwezo wa Mwenyezi Mungu kwa watu wenye kufikiri kwa akili zao, wakafikilia yakini yao.

التفاسير:

external-link copy
6 : 45

تِلۡكَ ءَايَٰتُ ٱللَّهِ نَتۡلُوهَا عَلَيۡكَ بِٱلۡحَقِّۖ فَبِأَيِّ حَدِيثِۭ بَعۡدَ ٱللَّهِ وَءَايَٰتِهِۦ يُؤۡمِنُونَ

Hizi Aya za Mwenyezi Mungu tunakusomea kwa haki; basi hadithi gani watakayo iamini baada ya Mwenyezi Mungu na Aya zake? info

Hizo ni Aya za Mwenyezi Mungu zinazo eleza uumbaji alio ufanya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya watu. Tunakusomea wewe katika Qur'ani kwa ulimi wa Jibrili, nazo Aya hizo ni za haki. Ikiwa hao hawaziamini hizi basi maneno gani watayasadiki baada ya maneno ya Mwenyezi Mungu, nayo ni Qur'ani na Aya zake

التفاسير:

external-link copy
7 : 45

وَيۡلٞ لِّكُلِّ أَفَّاكٍ أَثِيمٖ

Ole wake kila mzushi mwenye dhambi! info

Atapata maangamizo makubwa kila anaye mzulia Mwenyezi Mungu uwongo mbaya, na mwenye kukithiri madhambi yake kwa kitendo hicho!

التفاسير:

external-link copy
8 : 45

يَسۡمَعُ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ تُتۡلَىٰ عَلَيۡهِ ثُمَّ يُصِرُّ مُسۡتَكۡبِرٗا كَأَن لَّمۡ يَسۡمَعۡهَاۖ فَبَشِّرۡهُ بِعَذَابٍ أَلِيمٖ

Anaye sikia Aya za Mwenyezi Mungu akisomewa, kisha anashikilia yale yale aliyo katazwa, na anajivuna, kama kwamba hakuzisikia. Basi mbashirie adhabu chungu! info

Mzushi kama huyu husikia Aya za Mwenyezi Mungu akisomewa, nazo zinasema haki tupu. Kisha yeye huendelea na ukafiri wake kwa kutakabari, akaikataa Imani. Hali yake ni hali ya asiye pata kuzisikia Aya. Basi ewe Nabii! Mbashirie, kwa kumkejeli, kuwa atapata adhabu chungu kwa huko kushikilia kwake kitendo kitacho mletea adhabu hiyo.

التفاسير:

external-link copy
9 : 45

وَإِذَا عَلِمَ مِنۡ ءَايَٰتِنَا شَيۡـًٔا ٱتَّخَذَهَا هُزُوًاۚ أُوْلَٰٓئِكَ لَهُمۡ عَذَابٞ مُّهِينٞ

Na anapo kijua kitu kidogo katika Aya zetu hukifanyia mzaha. Watu hao ndio watakao kuwa na adhabu ya kufedhehesha. info

Na huyu mwenye inda, akijua kitu kidogo katika Aya za Mwenyezi Mungu huzifanya Aya zote za Mwenyezi Mungu ni kitu cha kufanyia maskhara na mzaha. Wazushi hao wingi wa madhambi watapata adhabu ya kuwadhalilisha kwa kiburi chao.

التفاسير:

external-link copy
10 : 45

مِّن وَرَآئِهِمۡ جَهَنَّمُۖ وَلَا يُغۡنِي عَنۡهُم مَّا كَسَبُواْ شَيۡـٔٗا وَلَا مَا ٱتَّخَذُواْ مِن دُونِ ٱللَّهِ أَوۡلِيَآءَۖ وَلَهُمۡ عَذَابٌ عَظِيمٌ

Na nyuma yao ipo Jahannamu. Na walio yachuma hayatawafaa hata kidogo, wala walinzi walio washika badala ya Mwenyezi Mungu. Na watapata adhabu kubwa. info

Nyuma yao ipo Jahannamu inawangojea, na walicho kichuma duniani hakitawapunguzia hata chembe ya adhabu yake. Wala hiyo miungu ya uwongo walio ifanya ndio ya kuwanusuru badala ya Mwenyezi Mungu, haitawakinga na chochote katika adhabu yake. Na wao watapata mateso makubwa, kwa kitisho chake na ukali wake.

التفاسير:

external-link copy
11 : 45

هَٰذَا هُدٗىۖ وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِـَٔايَٰتِ رَبِّهِمۡ لَهُمۡ عَذَابٞ مِّن رِّجۡزٍ أَلِيمٌ

Huu ni uwongofu. Na wale wale walio zikataa Ishara za Mola wao Mlezi watapata adhabu inayo tokana na ghadhabu iliyo chungu. info

Hii Qur'ani ni ushahidi kaamili wa Haki itokayo kwa Mwenyezi Mungu. Na hao wanao zikataa hoja zilio kusanywa na Qur'ani zilizo toka kwa Muumba wao na Mlezi wao watapata adhabu kali mno miongoni mwa namna za adhabu.

التفاسير:

external-link copy
12 : 45

۞ ٱللَّهُ ٱلَّذِي سَخَّرَ لَكُمُ ٱلۡبَحۡرَ لِتَجۡرِيَ ٱلۡفُلۡكُ فِيهِ بِأَمۡرِهِۦ وَلِتَبۡتَغُواْ مِن فَضۡلِهِۦ وَلَعَلَّكُمۡ تَشۡكُرُونَ

Mwenyezi Mungu ndiye aliye ifanya bahari ikutumikieni, ili humo zipite marikebu kwa amri yake, na ili mtafute fadhila yake, na mpate kushukuru. info

Mwenyezi Mungu peke yake ndiye aliye kufanyieni ikutumikieni bahari ili marikebu zipate kwenda juu yake kwa idhini yake, na uwezo wake, zikikubebeni nyinyi na bidhaa zenu, na ili mtafute kutokana na fadhila za Mwenyezi Mungu mali ya baharini kwa kupata manufaa ya ujuzi, na biashara, na jihadi, na zawadi, na uvuvi, na kutoa vyombo, na ili mpate kushukuru neema zake kwa kumsafia Dini Mwenyezi Mungu.

التفاسير:

external-link copy
13 : 45

وَسَخَّرَ لَكُم مَّا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِ جَمِيعٗا مِّنۡهُۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّقَوۡمٖ يَتَفَكَّرُونَ

Na amefanya vikutumikieni vilivyomo mbinguni na vilivyomo katika ardhi, vyote vimetoka kwake. Hakika katika hayo zimo Ishara kwa watu wanao fikiri. info

Na akakudhalilishieni vyote viliomo mbinguni, nyota zenye kung'ara na sayari, na vyote viliomo kwenye ardhi, makulima, mifugo, maji, moto, hewa, na jangwa, vyote hivyo vinatokana na Yeye Mtukufu, ili akuenezeeni manufaa ya uhai. Hakika katika hizo neema zilizo tajwa zipo Ishara zenye kuonyesha kudra yake kwa watu wenye kuzingatia Ishara.

التفاسير: