[41] Zakariya akamwomba Mola wake Mlezi amfanyie alama ya kuhakikisha bishara hii. Mwenyezi Mungu akamjibu: Alama yako ni kuwa hutaweza kusema na watu muda wa siku tatu, isipo kuwa utatumia ishara tu kuashiria utakacho. Na shikamana na dhikri ya Mwenyezi Mungu ukimtakasa na kumtukuza jioni na asubuhi.