[56] Na shikeni Swala kwa ukamilifu wa nguzo katika utulivu na unyenyekevu, ili ipate kuwa inazuia uchafu na mambo mabaya. Na wapeni Zaka wanao stahiki. Na mt'iini Mtume kwa yote anayo kuamrisheni, ili mpate kutaraji rehema ya Mwenyezi Mungu na radhi yake.