Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yao kwa mchezo. [16]
[16] Wala hatukuziumba mbingu na ardhi na viliomo baina yao kwa mpango huu wa hikima, na muundo huu wa namna peke yake, kwa mchezo. Bali tumefanya yote haya kwa hikima ya juu ambayo wanaifahamu wenye kuzingatia.