[74] Baada ya Nuhu tuliwatuma Mitume wengine wakilingania Tawhid, Upweke wa Mwenyezi Mungu, wakibashiria kheri na wakionya, na wakiungwa mkono na miujiza yenye kuonyesha ukweli wao. Watu wao wakawakanya kama walivyo kanya kaumu ya Nuhu. Haukuwa mwendo wa wapinzani kuwa wat'iifu, kwa sababu kule kukadhbisha kwao kulikuwa ni mbele kuliko kuzingatia na kupima. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu alipiga muhuri wa upotovu juu ya nyoyo za wale ambao mtindo wao ni kuzifanyia uadui hakika na Ishara zilizo wazi!