Na Mwenyezi Mungu anaita kwendea Nyumba ya Amani, na anamwongoa amtakaye kwenye Njia Iliyo Nyooka. [25]
[25] Na Mwenyezi Mungu anawaitia waja wake kwa Imani na vitendo vyema wendee Peponi, makao ya amani na utulivu. Na Yeye Subhanahu humwongoa amtakaye - kwa kuwa kesha jitayarisha vyema na kaelekea kheri - kwenye Njia ya Haki, nayo ni ya Salama.